Habari za Punde

RAIS KARUME ALIVUNJA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Amani Abeid Karume, alipokuwa akitoa hutuba yake ya kulivunja Baraza la Wawakilishi katika mkutano wa 21, huko katika ukumbi wa Jengo jipya la Baraza la Wawakilishi Chukwani leo.
Viongozi Waalikwa katika Mkutano wa 21, wa kulivunja Baraza la Wawakilishi uliofanyika jana katika ukumbi wa Baraza hilo liliopo Chukwani Nje ya Mji wa Zanzibar.

Baadhi ya waliokuwepo katika Mkutano wa 21 kulivunja Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pichani ni Waziri Kiongozi anaemaliza muda wake Shamsi Vuai Nahodha, Spika wa Baraza la Wawakilishi anaemaliza muda wake Pandu Ameir Kificho na mke wa Rais Mama Shadya Karume.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Amani Abeid Karume, akikagua Gwaride Rasmi lililoandaliwa kwa Ajili ya Ufungaji wa Kikao cha mkutano wa 21 wa Baraza la Wawakilishi, huko Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar jana.

1 comment:

  1. Asalam Alaikum mapara,

    Naona kila siku unatuwekea picha ulizopiga katika jengo jipya la baraza la wawakilishi ila sijaona hata picha moja inayoonesha sura ya jengo hilo kwa nje. Au hairuhusiwi kulipiga picha kwa nje? Tafadhali tuwekee hiyo picha inayoonesha sura nzima ya jengo linavyoonekana kwa mbali.

    Asante.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.