Habari za Punde

UFUNGUZI WA JENGO JIPYA LA BARAZA LA WAWAKILISHI - MBWENI


Mfadhi Sheikh Abdalla Mohammed Al Yuoseif akisoma risala ya jumuiya ya iliofanikisha ujenzi huo na kutowa shukrani kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufanikisha ujenzi huo.

Wageni waalikwa katika uzinduzi wa jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni.


Katibu wa Baraza Ibrahim Mzee akisoma risala ya kiufundi ya ujenzi wa jengo la Baraza.
Waandishi wa habari wakifuatilia hutuba katika sherehe za uzinduzi wa jengo jipya la Baraza la Wawakilishi Mbweni.
Wananchi wakihughuria uzinduzi wa jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Amani Abeid Karume akimsikiliza Katibu wa Baraza Ibrahim Mzee akitowa risala ya kiufumdi ya ujenzi wa baraza hilo, kushoto Sheikh Al- Youseif na kulia Spika wa Baraza Pandu Ameir Kificho.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akikabidhiwa ufunguo wa Jengo jipya la Baraza la Wawakilishi na Mfadhiri wa jengo hilo Sheikh Abdalla Mohammed Al-Youseif, baada ya uzinduzi wake huko Mbweni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. kutoka kushoto Waziri Kiongozi Mstaafu Mohammed Gharib Bilal, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Spika Pandu Ameir Kificho, Rais wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, Mfadhili Sheikh Abdalla Mohammed Al-Youseif, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume.
Waziri Kiongozi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha na Balozi wa Saudia Ali AL- Jarbou wakibadilishana mawazo nje ya jengo la baraza.
Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad akibadilishana mawazo na Mfadhili wa ujenzi huo na Balozi wa Saudia Tanzania Ali Al-Jarbuo baada ya kuzinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho (katikati) akiwa na balozi wa Saudia Nchini Tanzania Ali Al-Jarbuo kushoto na kulia Mhisani wa Ujenzi huo Sheikh Abdalla Mohammed Al-Youseif wakibadilishana mawazo baada ya ufunguzi wa Jengo la Jipya la Baraza la Wawakilishi Chukwani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.