Kuna mdau ameuliza suala kuhusiana na mchezaji huyu wa zamani aliyewahi kuzichezea timu za Small Simba, Mlandege, timu ya taifa ya Zanzibar na Taifa Stars katika miaka ilee.
Kumbukumbu yake anasema alimkumbuka mchezaji huyu siku alivyowatungua Waarabu wa Algeria katika mchezo mkali uliofanyika uwanja wa Taifa na huku akilinganisha matokeo ya sare ya Taifa Stars dhidi ya Waalgeria ambapo Abdi Kassim Babi aliipatia Timu yetu bao la kuongoza kwa free kick murua yenye hadhi ya kubaki katika kumbukumbu za kihistoria.
Kuna mdau yeyote ana taarifa za mchezaji huyu wa zamani yupo wapi na anafanya nini sasa?
Juma Bakar Kidishi mara ya mwisho nikiwa zanzibar nilimuacha akiwa anaendelea na shughuli zake za kibiashara(ujasiriamali).
ReplyDeleteKatika shughuli za michezo bado yupo katika benchi la ufundi la timu ya Malindi akiwa na wakali wa enzi zake kama Amour Aziz "kijeba", Ali Shariff "Adolf" n.k
Nimeondoka zanzibar karibu miaka miwili sasa,sijuwi kama bado yupo zanzibar na kama bado anaendelea na shughuli hizo.
Tatizo nimeliona katika hoja ya muulizaji, ambayo ni muhimu sana, ni kuwa wakali hawa wa enzi zao wanasahauliwa sana.
Vyama vya soka AFA, TFF, hawana hata takwimu za uhakika zinazowahusu kama mechi walizocheza (cap)katika timu ya taifa an vilabu, magoli waliyofunga na mafanikio yao kisoka.
Michango yao ni muhimu kuwekwa katika kumbukumbu kwa kuwa inachangia kuakisi maendeleo ya soka tuliko toka na tunakokwenda (fifa). Kadhalika, wakali hawa wanapaswa kupewa role katika timu za vijana ili ujuzi wao urithiwe na vijana wanaochipukia. Tumeona wenzetu wanavyowatumia wachezaji zamani kuendeleza soka...makocha wanaokuja saivi ulaya wengi ni wachezaji wa zamani na wamekuwa na mafanikio makubwa mfano Rijkaard, Gullit, Guardiola, Cruyyf, Bruce, Southgate n.k
Hii muhimi kwetu pia, tukumbuke enzi za akina "Kidishi" ndiyo enzi ambazo mpira wa uhakika ukichezwa Zanzibar, viwanja vikifurika watu na upinzani wa soka ulikuwa mkali sana kadhalika uwezo wa wachezaji hao ulikuwa mkubwa kuliko wa sasa.
Hivi sasa soka limeporomoka kwa mengi tu, huenda tukiwatumia hawa wakali wa zamani kutowa mchango wao katika kuongoza FA na timu za soka huenda hali ikabadilika.
Mdau Misri
Ahsante Mdau mawazo yako yako kwenye mstari.
ReplyDeleteNilikuwa najaribu kufuatilia maendeleo ya kijana wetu Ali Badru ambae yupo Misri akisakata kabumbu la kulipwa huko Ismaailiya.
Tumeambiwa anachezea timu ya Al Canaal.
Mlioko Misri mnaweza kutupa taarifa zozote juu ya klabu na vipi maendeleo yake tokea afike huko
Tunawasikiliza
Mdau kusema kweli kijana yupo na hajaanza bado kucheza rasmi, ndiyo kwanza anazowea mazingira na wenzake.
ReplyDeletekwakweli amekuwa gumzo klabuni kwake na washabiki wa timu hiyo, ambao wamesikia sifa zake kutoka mashindano ya kimataifa aliyoshiriki Ali.
Mimi ni miongoni mwa wazanzibar niliyefarijika sana na ujio wake.
Tatizo lililokuwapo ni moja ambalo ni la msingi sana.
Ali, tumepata taarifa kuwa amekuja hapa bila ya uwakilishi mzuri (free agent) sina hakika na hili naomba muulizie zaidi. Maana yake amejiunga na soka la kulipwa akiwa hana wakala aliyesajiliwa (unregistered agent) hii ni hatari kwake na kwa mustakbali wake.
Ali ni kijana mzuri, ameshazungumzwa sana na magazeti ya hapa na kwakuwa kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar anamjuwa imekuwa rahisi kwake kujitangaza zaidi.
Hii ya kuja mtupu mtupu kwa uwakala wa kienyeji ni hatari na hapa Misri imeshawaliza vijana wengi.
Kuna sakata hapa linaendelea baya sana kuhusu uwakala wa mchezaji mmoja wa Zambia anaitwa Kalaba.
Ni kijana mdogo anacheza kiungo, timu ya taifa ya Zambia, kama umetizama AFCON ya Angola, alikuwa akivaa jezi namba 17.
Alikuwa anachezea timu moja nimesahau jina lake ya Uturuki, amemaliza mkataba wake na mawakala wa Misri wakamtaka ajiunge na Al Ahly, wakati akijuwa kuwa anajiunga na vigogo hao wa soka barani Afrika.
Mawakala hao walishachukuwa pesa za timu nyingine Ismailiya na kumtaka akacheze huko, Kalaba amegoma akitaka timu aliyokubaliana mwanzo ya Al Ahly.
Sakata bado bichi kwa kuwa kijana yupo Lusaka hana timu (clubless).
Sakata hili linatokea amid information kuwa Ali Badru amejiunga na Al Canal bila ya wakala anayejuulikana (registered agent) hivyo, anaweza kuwalizwa na kuharibiwa future yake na wajanja.
Kilichonishangaza ni taarifa kuwa si kuwa Zanzibar kama hakuna wakala waliosajiliwa na Fifa, bali ni ujinga au ukosefu wa uelewa wa masuala ya soka la kulipwa wa Ali Badru na wazee wake au timu yake ya Jamhuri.
Ndg. Mapara kama wewe mwandishi na mwanamichezo, ningeomba suala hili ulisukume kwa viongozi wa michezo na vyombo husika wa kuweka kanuni za kuwalinda vijana wanaopata nafasi ya kucheza soka la kulipwa.
Iwepo kanuni ya lazima kuwa mchezaji lazima awakilishwe na wakala au mwanasheria, ili haki zake zilindwe. Vinginevyo anaweza Ali Badru akapata matatizo (Mungu amuepushie) akawa hana mtu wa kumsimamia, ukitilia maanani waarabu hawaaminiki wakiwa kwao huku.
Hawawezi kumtafutia interests club, interest contracts, ambazo ni wakala mahiri tu anaweza kuzisimamia na si mtu hivi hivi tu. Nampongoza Ali Badru, ameshafunguwa milango kwa vijana wengine, kwani kuna uwezekano mkubwa kuwa kuwa vilabu vingine vya Misri vikaja kutafuta vipaji zaidi huko nyumbani, hii nikwasababu walikuwa hawaijuwi Zanzibar, kwa kufichwa kwake kisiasa na kimataifa.
Sasa wametambuwa kuwa kuna Zanzibar ambayo ina vijana siyo tu wanaweza kucheza mpira bali hata maadili na silka zao(kiimani) zinafanana na za Misri, hivyo ni rahisi kuzowea mazingira na utamaduni sare na wa kwao.
Mdau Misri
Mimi si mwandishi wa makala za michezo ila ujumbe wako nitaufikisha kwa mwandishi wetu wa michezo Salum Vuai kwa kuchukua hatua zaidi.
ReplyDeleteAhsante sana Mdau kutoka Misri.