
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar Baada ya kupiga kura katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akipiga kura katika kituo cha skuli ya Kiembesamaki..

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akipiga kura katika kituo cha skuli ya Kiembesamaki akipiga kura yake.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akiwa katika kituo cha Kupigia kura cha Skuli ya Kiembesamaki.

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia CUF akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kupigakura.

MGOMBEA Urais kupitia Chama cha CUF Seif Sharif Hamad akipida kura yake.

MGOMBEA Urais kupitia Chama cha CUF Seif Sharif Hamad akichukuwa Shahada yake ya kupigia kura katika kituo cha Skuli ya Mto Pepo Daraja Bovu.

MGOMBEA Mwenza wa Rais wa Tanzania kupitia Chama cha CCM Mohammed Gharib Bilal akipiga kura jana.

MGOMBEA Mwenza wa Rais wa Tanzania kupitia CCM Mohammed Gharib Bilal akipiga kura katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki.

MGOMBEA Urais kupitia Chama cha TADEA Juma Ali Khatib akiwaonesha waandishi wa habari kura yake ya Urais kabla ya kuitumbukiza katika kisanduku cha kupigia kura katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki.

MGOMBEA Urais kupitia Chama cha TADEA Juma Ali Khatib akipiga Kura yake katika Kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Kiembesamaki.


MWANANCHI akionesha kitambulisho chake cha kupigia kura kwa Afisa wa Tume ya Uchaguzi katika kituo cha Skuli ya Kijito Upele Jimbo la Mwanakwerekwe.


HATA na mimi nina haki yangu ya kupiga kura ndivyo inavyoonekana akisema mzee huyu akipiga kura yake kutimiza demokrasia yake akiwa katika kituo cha skuli ya Bwejuu.

AFISA wa Uchaguzi wa Kituo cha Skuli ya Bwejuu akiangalia majina ya wapiga kura wa kituo hicho katika daftari la wapiga kura.

WANANCHI wa Kijiji cha Bwejuu wakipiga kura kumchagua Kiongozi wao. waklitumia Demokrasia yao.

WAANDISHI wa Habari wa Vyombo mbalimbali wakiwa makini kupiga picha ilio bora wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akipiga kura kituo cha Kiembesamaki.

WANANCHI wa Kijiji cha Makunduchi wakisubiri kupiga kura.

MWANANCHI wa Kijiji cha Bwejuu Jimbo la Muyuni akipiga kura yake katika kituo cha skuli ya Bwejuu.

MKAAZI wa Kijiji cha Kitogani akipiga kura yake jana.

WANANCHI wa Kijiji cha Kitogani wakiangalia majina yao kuona kituo chao cha kupigia kura katika skuli Kitogani.

WANANCHI wa Jimbo la Mji Mkongwe wakiwa katika foleni huku mvua ikinyesha wakisubiri kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura katika kituo cha skuli ya Vikokotoni.

MAWAKALA wa Vyama vya Siasa wa Jimbo la Mji Mkongwe katika kituo cha skuli ya Haile.

MAWAKALA wa Vyama vya Siasa wakipitia majina ya wapiga kura katika Daftari la Wapiga Kura katika Kituo cha kupigia kura Skuli ya Kiembesamaki.

WANANCHI wa Jimbo la Kiembesamaki wakiwa katika mstari kusubiri kupiga kura yao kutimiza haki yao ya kumchaguwa wamtakaye, katika uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment