Habari za Punde

ZANZIBAR HEROES YALALA 1-0 DHIDI YA IVORY COAST

 Mshambuliaji wa Ivory Coast Kipre Tchetche akichuana na Beki wa Zanzibar Heroes Aggrey Morris
 Mshambuliaji aliyeacha jina wa Zanzibar Heroes Ally Ahmed "Shiboli" akikata mbuga baada ya kumuacha beki wa Ivory Coast
Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakienda mapumzikoni baada ya kumalizika kipindi cha kwanza
Piucha kwa hisani ya John Bukuku @ fullshangwe.blogspot.com
Timu yetu ya taifa Zanzibar Heroes leo imewasononesha wapenzi wake kwa kufungwa bao moja bila ya majibu katika mchezo wa pili dhidi ya timu alikwa ya Ivory Coast.


Goli la Ivory Coast lilipatikana katika kipindi cha pili baada ya timu zote kwenda mapumziko bila ya kufungana.

Washambuliaji wa Zanzibar Heroes itabidi wajilaumu wenyewe kwa kukosa nafasi nyingi za wazi walizopata hasa katika kipindi cha pili.

Kocha wa Zanzibar Heroes, Stewart Hall aliisifu timu ya Ivory Coast na alisema Zanzibar Heroes iliwaheshimu sana kwani ilianza mchezo kwa taratibu na hivyo kuwapa nafasi timu pinzani kuutawala mchezo huo.

Katika mchezo mwengine kati ya Sudan na Rwanda matokeop yalikuwa sare isiyo na magoli na hivyo timu zote nne zilizo katika kundi hili kuwa na nafasi ya kuendelea katika hatua ya robo fainali.

Rwanda inahitaji sare tu kuweza kuendelea ila Zanzibar inahitaji kushinda mchezo wa mwisho kwani sare haitowapa uhakika wa kuendelea katika michuano kwani itategemea na matokeo ya mchezo kati ya Sudan na Ivory Coast.

Mechi za mwisho zinatarajiwa kuchezwa tarehe 3/12/2010.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.