Habari za Punde

JUISI YA NA NANASI NA UKWAJU

Vinavyohitajika


Ukwaju 100g

Sukari 200g lakini utaangalia kiasi ukipendacho

Arki ya portessa flavour kijiko 1 cha chai (arki hii ni maarufu inapatikana Afrika)

Nanasi kama likiwa dogo 1 au nusu kama kubwa

Namna ya kutayarisha na kutengeneza

Roweka ukwaju na sukari kwa maji ya moto na uwache kwa nusu saa.

Menya nanasi na ulisage kwenye blender ili upate juice.

Weka pembeni juice ya nanasi.

Saga ukwaju kwenye blender pamoja na sukari uliyoiroweka.

Ichuje juice hiyo ya ukwaju na nanasi.

Changanya juice hizo mbili na umalizie kwa kuweka arki.

Koroga vizuri na weka barafu na tayari kwa kunywewa.

Kidokezo

Unaweza kuigandisha ikawa barafu na ukaiblender ikawa kama smoothy (zito zito), pia unaweza kufanya juice hii ya ukwaju kwa kuchanganya na tunda la peach inakuwa na ladha nzuri.

2 comments:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.