Habari za Punde

MAMBO YA MKUTANO WA MSWADA WA MABADILIKO YA KATIBA UKUMBI WA SKULI YA HAILE -SELASSI

 MWENYEKITI wa Mkutano wa Mswada wa Mabadiliko ya Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jadi Simai Jadi, Mbunge wa Mkwajuni akifuatilia michango ya Wananchi wakichangia kushoto Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta.      



MWANANCHI akichangia maoni yake katika mkutano wa Mswada wa Katiba uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Haile.
 WAJUMBE wa Mkutano wa Mswada wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia michango ya Wananchi wanayoitowa katika ukumbi huo. 
WANANCHI waliofika katika ukumbi wa mkutano wa kujadili mswada wa Katiba ya uliofanyika ukumbi wa skuli ya sekondari ya Haile, wakifuatilia mjadala huo.   
 WANANCHI wakiwa katika Vikundi baada ya Mkutano huo kuahirishwa baada ya mmoja wa Wachangia mada katika mkutano huo kuchana mswada huo katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Haile.
 WANANCHI wakijadiliana mambo nje ukumbimbi wa Mkutano baada ya kuhairishwa mkutano huo kabla ya muda wake kutokana na mmoja wa Mwananchi kuuchana Mswada huo.  
MWANANCHI akitowa maono yake kutokana na kuvunjika kwa mkutano huo akizungumza na mwandishi wa habari nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kuhairishwa.

1 comment:

  1. msemakweli mpenzi wa Mungu wazanzibari tumechoshwa na dharau za serikali ya Muungano sasa tunaomba mutuache tupumue ,kila siku tunafanyiwa danganya toto kwa kuambiwa kuna marekebisho kumbe madhambi ya katiba yamezidi na sasa hatudanganyiki teeeeeeeeeeeeeeena .
    Wazanzibar tumeamka.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.