WAZIRI wa Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Abdilah Hassan Jihad akimkabidhi Seti ya Jezi Katibu wa ZFA Wilaya ya Mjini Yahya Juma kwa ajili ya mchezo wa Fainali leo na timu ya Mkoa wa Kaskazini, hafla hiyo uimefanyika Hoteli ya Mazsons Shangani.
WAZIRI wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdilah Hassan Jihad akimkabidhi Vifaa vya Michezo kwa timu ya Wilaya ya Mjini kwa Katibu wa ZFA Mjini Yahya Juma .
WAZIRI wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdilah Hassan Jihad akimkabidhi jezi Mjumbe wa ZFA Mkoa wa Kaskazini Unguja Kombo Sheha kwa ajili ya timu yake katika mchezo wa Fainal unaofanyika leo Uwanja wa Mao.
WACHEZAJI wa Wilaya ya Mjini na Kaskazini wakiwania mpira katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Mufindi Muungano Cup uliofanyika uwanja wa Mao timu ya Wilaya ya Mjini imeshinda 3-1
MCHEZAJI wa timu ya Mkoa wa Kaskazini Othman Haji akimpita beki wa timu ya Wilaya ya Mjini Mohammed Hassan katika mchezo wa Fainali ya kombe la Mufindi Muungano Cup iliofanyika uwanja wa Mau tim u ya Wilaya ya Mjini imeshinda 3-1
WACHEZAJI timu ya Wilaya ya Mjini wakimbeba juu Katibu wa ZFA Wilaya ya Mjini Yahya Juma baada ya timu yao kuifunga timu ya Kaskazini Unguja kwa mabao 3-1
WACHEZAJI wa timu ya Wilaya ya Mjini wakishangilia ushindi wao dhidi ya timu ya Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kuifunga katika mchezo wa Fainali uliofanyika Uwanja wa Mao
No comments:
Post a Comment