Habari za Punde

SUZA YAPATA BARAZA JIPYA

Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ramadhan Abdulla Shaaban amewateuwa wajumbe wapya wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
 

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mwanaidi Saleh Abdulla, Waziri Shaaban amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa sheria namba 8 ya mwaka 1999 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kifungu cha 12(d).

 Walioteuliwa kuwa wajumbe wa Baraza hilo ni Said Mohammed Said Mwakilishi kutoka Baraza la Wawakilishi, Dk. Narman Saleh Jiddawi kutoka Taasisi ya Sayansi ya Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Simai Mohammed Said ambae ni mfanyabiashara, Amina Khamis Shaaban Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar, Khamis Mussa Omar Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na Mwanaidi Saleh Abdulla Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali.

Wengine ni Dk. Zakia Mohamed Abubakar, kutoka SUZA,  Mmanga Mjengo Mjawiri kutoka SUZA, Maulid Omar Haji kutoka SUZA, Profesa Mustafa Roshash Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar na Mtumwa Ali Ameir Mwenyekiti wa Serikali ya Wanafunzi SUZA.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, Hassan Nassor Moyo ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Uteuzi huo umeanza tarehe 15 Juni mwaka huu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.