Habari za Punde

BALOZI SEIF AKUTANA NA MWAKILISHI MAALUM WA UN OFISINI KWAKE

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisalimiana na Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bibi Marta Santos Pais

Makamu wa Pili wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Mwakilishi  maalum wa umoja wa Mataifa

Ipo haja kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kuangalia uwezekano wa kuanzisha mafunzo maalum kwa wanafunzi Maskulini ambayo yatasaidia elimu ya kujikinga dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mapambano dhidi ya ukatili kwa watoto Bibi Marta Santos Pais ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.


Bibi Marta amesema udhalilishaji wa Kijinsia hasa kwa watoto wadogo unaathiri ustawishaji wa watoto hao jambo ambalo kama hakukuandaliwa mipango madhubuti hasa ya kielimu ongezeko la vitendo hivyo litazidi.

Amesema umoja wa Mtaifa Kupitia Shirika lake la Kuhudumia watoto la UNICEF utajitahidi kuendelea kutoa misaada ili kukomesha vitendo hivyo vinavyokwenda kinyume na Haki za Binaadamu.

Bibi Marta ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kuyaweka makundi ya vijana, Wanawake na Watoto katika Wizara moja. Amesem jambo hilo litasaidia kuratibu mwenendo mzima wa makundi hayo katika kuyapatia huduma zinazostahili. Akitoa shukrani zake kwa juhudi za Umoja wa Mtaifa katika kusaidia Maendeleo ya Zanzibar Balozi Seif amesemA Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuhakikisha tabia ya udhalilishwaji wa watoto nchini inapigwa vita na jamii yote.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekutana na Balozi wa Japan Nchini Tanzania bwana Safaguchi aliyefika Ofisini kwake kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi Nchini Tanzania. Balozi Seif Ameipongeza Japan kwa kuwa Mshirika wa karibu wa Tanzania katika kusaidia maendeleo ya Jamii hasa katika masuala ya maji na elimu yaliyopelekea kupunguza matatizo kadhaa yanayowakabili Wananchi. Naye Balozi wa Japan Nchini Bwana Safaguchi amezipongeza jitihada za Viongozi wa Tanzania zilizopelekea kutekelezwa vyema majukumu yake.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/9/2011.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.