Habari za Punde

BALOZI SEIF AWASILI MAREKANI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewasili Mjini Washington DC Nchini Marekani kuanza ziara ya Kiserikali ya siku nane Nchini humo.

Balozi seif anafanya ziara hiyo kwa mwaliko wa Shirika la Uwekezaji Vitega Uchumi Afrika la Nchini Marekani.

Lengo la ziara hiyo ni kuitangaza Zanzibar kwa Taasisi na Mashirika mbali mbali ya Uwekezaji Nchini Marekani kuangalia uwezekano wa kuwekeza miradi yao ndani ya Zanzibar.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi amefuatana na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais anayeshughulikia Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Mh. Omar Yussuf Mzee, Waziri wa Nchi Afisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Ftma Alihabib Fereji na Naibu Waziri wa Afya Mh. Sira Ubwa Mamboya.

Wengine ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Magomeni Mh. Salmin Awadh Salmin, Katibu mkuu Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Nd. Julian Raphael, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Khamis wakiwemo baadhi ya Wafanyabiashara wa Zanzibar.

Balozi Seif anatarajiwa kuondoka Washington Marekani tarehe 6 Novemba mwaka huu kurejea nyumbani akiuacha ujumbe aliofuatana nao kumaliza ziara za kukutana na wawekezaji wa Marekani.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.