WAZIRI wa Biashara Viwanda Masoko Nassor Mazrui akijibu hoja za Wafanyabiashara katika Mkutano wa Sita wa Baraza la Biashara Zanzibar uliofanyika ukumbi wa Salama Bwawani.
BAADI ya Washiriki wa Mkutano wa ZBC wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Biashara Dk .Ali Mohamed Shein.
MAKATIBU Wakuu wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Biashara Zanzibar wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano.
MAOFISA wa Mabenki zilioko Zanzibar wakifuatilia Mkutano wa Sita wa Baraza la Biashara Zanzibar.
BAADHI ya Wafanyabiashara ya Sekta ya Utalii Zanzibar wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano Bwawani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akimsikiliza Ofisa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar, akielezea moja ya bidhaa za Wajasiriamali, mafuta ya kokwa ya ubuyu. yanayosaidia kuweka sawa virutubisho mwilini na kuongeza nguvu na kutibu maradhi ya mifupa na sukari.
RAIS wa Zanzxibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Rais wa Ushirika wa Vitega Uchumi Afrika Daniel Anagho, Waziri wa Biashara Zanzibar Nassor Mazrui wakiangalia bidhaa zitokanazo na Mnazi katika maonesho ya Wajasiri Amali yaliofanyika Viwanja wa Bwawani Hoteli.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyakiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuelezea Rais wa Ushirika wa Vitega Uchumi Afrika Daniel Anagho, mooja ya bidhaa za Wajasiriamali ya mafuta ya kurutubisha Nywele na maradhi ya ngozi.
WASHIRIKI wa maonesho ya Wajasiriamali wakiwa katika maonesho hayo ya kuonesha jitihada zao za uzalishaji mali kwa kutumia malihafi ya Zanzibar.
OFISA wa Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto Saida Ali Mohammed akimuelezea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein moja ya bidhaa za Wajasiriamali alipotembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa zao wakati wa mkutano wa sita wa Baraza la Biashara Zanzibar.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia bidhaa za Wajasiriamali katika maonesho yao yaliofanyika viwanja vya Bwawani Hoteli.
No comments:
Post a Comment