Habari za Punde

BALOZI SEIF AZUNDUA PROGRAMU YA MIUNDO MBINU YA MASOKO, UONGEZAJI THAMANI NA HUDUMA ZA FEDHA VIJIJINI

Washiriki Wa Mkutano Wa Uzinduzi Wa Programu Ya Miundo Mbinu Ya Masoko, Uongezaji Thamani Na Huduma Za Kifedha Vijijini.

Ushiriki Huo Pia Umehusisha Baadhi Ya Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi Wa Smz Na Smt Pamoja Na Wadau Wa Sekta Za Kilimo, Uvuvi, Biashara Na Wajasiri Amali Wadogo Wadogo Hapa Zanzibar.

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akizindua Programu Ya Miundo Mbinu Ya Masoko, Uongezaji Thamani Na Huduma Za Kifedha Vijijini Katika Ukumbi Wa Salama Huko Hoteli Ya Bwawani Mjini Zanzibar.


Wakati Sekta ya Kilimo ambayo ndio tegemeo kubwa la Taifa kwa kutoa ajira zaidi ya asilimia 70% ya Wakulima bado Wakulima wengi wanakabiliwa na changamoto kadhaa katika uzalishaji wa mazao yao.

Akizindua Programu ya Miundo mbinu ya masoko, Uongezaji thamani na Huduma za Kifedha Vijijini hapo katika ukumbi wa salama Bwawani Makamu wa Pili wa Ris wa Zanzibar Balozi Seif amesema wakulima wengi wamekuwa wakizalisha chakula katika kiwango duni, ukosefu wa masoko na hata uwezomdogo wa kujiwekea hakiba.


Balozi Seif alisema Sekta ya Kilimo hivi sasa inachangia asilimi 50% ya chakula kinachotumika hapa Zanzibar.
Alisema Serikali inaendelea kuchukuwa hatua za kuimarisha miundo mbinu ya umwagiliaji, kuongeza ruzuku ya pembejeo na utekelezaji wa Program tofauti kwa lengo la kuendeleza huduma za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

“ Programu ya { MIVARF } ninavyoizindua leo ni mojawapo ya juhudi za Serikali kuwawezesha Wakulima hasa Vijijini kukabiliana na baadhi ya changamoto zinazowakabili ili waongeze tija, kipato na kuwa na uhakika wa upatikanaji wa Chakula ”. Alifafanua Balozi Seif.

Alifahamisha kwamba Programi hii ni mwenendo wa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Programu mbili zilizopita ambazo zilitekelezwa upande wa Tanzani Bara katika kipindi cha mwaka 2002 hadi 2010.

Balozi Seif alisema jumla ya shilingi Bilioni 151.43 zilitolewa mikopo kwa wastani wa wanachama 48,266 katika kipindi cha miaka sita ambao idadi kubwa zaidi ya wanawake waliomo katika vikundi vha hakiba na Mikopo.

Alisisitiza kwamba Wananchi wengi waliowezeshwa kupitia Programu hii wamebadili maisha yao kwa kujenga nyumba bora, uhakika wa chakula na kujiwekeza hakiba kutokana na kutumia mbinu za kisasa za uzalishaji katika kilimo chao.

Balozi Seif ameipongeza Serikali ya Muungano, Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo { IFAD }, Benki ya MAaendeleo ya Afrika

{ ADB }, Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani Afrika { AGRA }kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza Programu hiyo.

Alisema amefarajika kuona Lengo la Programu hii ni kuchangia jitihada za Serikali katika kupiga vita Umaskini kwa kuongeza kipato na uhakika wa chakula kwa kutumia njia za kudumu.

Mapema Mratibu wa Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijinini hapa Zanzibar bwana Halfan Masoud Saleh alisema Programu hiyo mbali ya wakulima pia itahusisha Wavuvi, Wafugaji, Wafanyabiashara na Wajasiri amali wadogo wadogo.

Akitoa shukrani zake Katibu Mkuu Afisi ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Limo amesema uanzishwaji wa Programu hiyo kwa kujumuisha Pande zote mbili utatoa fursa zaidi ya kuimarisha Muungano.

Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na huduma za Kifedha Vijijinini utakaochukuwa Miaka saba unatarajiwa kugharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 170.


Othman Kahmis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
29/11/2011.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.