KATIBU wa CCM Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, Shukuru Adam Ali, akimkabidhi fomu ya kugombea Nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Uzini, Mhe.Mohammed Raza, kugombea Jimbo hilo ambalo liko wazi kutokana na Kifo cha aliyekuwa Mwakilishi jimbo hilo Mwalim Mussa Khamis Silima.
Mfanyabiashara na Mwanasiasa Mhe. Mohammed Raza akiwaonesha waandishi wea habari fomu yake ya kugombea Uwakilishi wakati akikabidhiwa na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kati Shukuru Adam, uchukuwaji wa fomu hizo unafanyika katika Ofisi ya CCM Dunga.
Waandishi wa habari mbalimbali wakishuhudia uchukuwaji wa Fomu za wagombea Uwakilishi wa Jimbo la Uzini, katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Kati Unguja Dunga.
Mfanyabiashara na Mwanasiasa Mohammed Raza, akizungumza na Waandishi wa habari matarajio yake kama atapata ridhaa ya Wananchi kumchagua mambo atakayofanya Jimboni.mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Palace Malindi Zanzibar.
No comments:
Post a Comment