MLINZI wa timu ya Zanzibar heroes Aggrey Moris akifunga bao la tatu katika mchezo wao na Somalia katika kinyang’anyiro cha kuwania kombe la tusker challenge uliochezwa jana jijini Dar es Salaam
MLINZI wa Zanzibar Heroes Aggrey Moris akimdhibiti mshambuliaji wa Somalia Abdulaziz Mohamed wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa kuwania kombe la Tusker challenge uliochezwa jana katika uwanja wa taifa
MCHEZAJI wa timu ya Taifa ya soka Zanzibar Amir Hamad kulia aliangalia namna ya kumpita kipa wa Somalia Khalid Ali katika mchezo wao wa kuwania kombe la Tusker challenge uliochezwa jana uwanja wa taifa jijini Dar ambapo Heroes iliibuka na ushindi wa mabao 3- 0
KOCHA Mkuu wa timu ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroko kulia akipeana ushauri msaidizi wake Steewart John Hall wakati timu yao ilipokua ikipambana na Somalia ambapo iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-0
SULEIMAN Kassim wa Zanzibar Heroes kulia akitafuta mbinu ya kumpita mlinzi wa somalia Abdulkadir Ali katika pambano la kuwania kombe la Tusker Challenge katika pambano hilo Zanzibar iliibuka na ushindi wa mabao 3-0
MCHEZAJI wa timu ya Somalia Mohamed Abdinur akiwa na mpira langoni mwa Zanzibar Heroes huku kipa wa Heroes Mwadini Ali akiwa makini kumdhibiti mchezaji huyo katika mchezo wao wa kuwania kombe la Tusker uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar jana
ABDUL HALIM Ali wa Zanzibar Heroes akipambana na mlinzi wa Somalia Said Mohamed katika mchezo wa kuwania kombe la Tusker challenge uliochezwa jana katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ambapo Zanzibar ilishinda mabao 3-0.
Picha zote na Haroub Hussein
No comments:
Post a Comment