Mchezaji wa timu ya KmKm Tizzo Charles, akimpita mchezaji wa timu ya Kikwajuni Male Ali katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Mao.timu ya Kikwajuni imeshinda kwa mabao 5--2
Mchezaji wa timu ya Kikwajuni Ramadhani Hussein mwenye jezi nyekundu na mchezaji wa timu ya Kmkm Mahammed Ali wakiwania mpira katika mchezo wa ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Mao timu ya Kikwajuni (Sauti ya Tembo) imeshinda 5--2
Mchezaji wa timu ya Kmkm Amour Kassim, akiokoa mpira golini kwake heri ya lawama kuliko fedhaha, wakati timu yake ikiwa imeshalala kwa mabao 5--2
Mchezaji wa timu ya Kmkm Hashim Ramadhani, akizuiya mpira huku beki wqa timu ya Kikwajuni akijiandaa kumzuiya asilete madhara golini kwake.
Mchezaji mwenye makeke awapo uwanjani Ame Kibobea, akijiandaa kumpiga chenga beki wa timu ya Kikwajuni.
Mashabiki wa timu ya Kikwajuni wakishangilia timu yao ilipoandika goli la tano na la kufunga kitabu cha magoli kwa masarahani wa timu ya Kmkm.kikwajuni imeshinda 5--2
No comments:
Post a Comment