Na John Gagarini, PWANI
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza amesema sio kweli kuwa wanafunzi kuwekwa lebo kuwa ni wale wenye matatizo makubwa ya kiafya na kuwa ndio wenye kuishi na virusi vya UKIMWI.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mjini Kibaha na kusema kuwa habari hizo si za kweli.
Mahiza alisema kuwa anapingana na wale wote waliosema kuwa wanafunzi hao wamewekewa alama kwani serikali haiwezi kufanya kitendo kama hicho.
“Tumesikitishwa na wale wote waliosema hivyo kwani jambo hili limetufedhehesha na serikali haiwezi kuwawekea alama kwani wanafunzi walioathirika wako lakini kitu hicho hakiwezi kufanyika kwani itakuwa ni kuendeleza unyanyapaa,” alisema Mahiza.
Alisema wazazi wa wanafunzi hao walikubaliana watoto wao kuwa na alama na kuona kuwa hawakuona ubaya wowote lakini si kama ilivyotafsiriwa na baadhi ya watu wakiwemo wanaharakati wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.
“Mwanafunzi mwingine anasoma shule ya Msingi Kongowe ambaye alifariki juzi yeye anasumbuliwa na ugonjwa wa mtindio wa ubongo lakini si kweli kuwa wanaovalishwa ni wale walioathirika na ugonjwa wa UKIMWI”, alisema Mahiza.
Alisema kuwa kutokana na taarifa hizo mashirika ya haki za binadamu duniani yalipiga simu kuiuliza serikali kama inatekeleza suala hilo.
Hivi karibuni baadhi ya wanaharakati walisema kuwa baadhi ya skuli imewawekea lebo wanafunzi ambao wanaishi na virusi vya ugonjwa wa UKIMWI.
No comments:
Post a Comment