Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa ndani ya Mjengo wa kutunga Sheria, wakiwa katika Kikao cha Asubuhi wakiendelea na uchanguaji wa Marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma.inayoendelea kujadiliwa na Wajumbe katika Ukumbi huo wa Mkutano.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza wakipitia Mswada wa marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma.ikichangiwa na wajumbe katika ukumbi wa mkutano.
Mwakilishi wa Kitope Mshimba Makame akichangia marekebisho ya Sheria ya Utumisha wa Umma ilipokuwa ikichangiwa na Wajumbe katika vipengele vilivyorekebisha.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salimin Awadh, nae akichangia marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma, katika mkutano wa Baraza la Wawakilishi unaoendelea kujadili marekebisho hayo leo katika kikao cha asubuh.
Mwakilishi wa nafasi za Wanawake Asha Bakari Khamis, akichangia katika mkutano wa baraza la Wawakilishi kupitisha Miswada iliowakilishwa katika mkutano huo unaoendelea katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Wawakilishi wakitoka katika Ukumbi wa Mkutano baada ya kumalizika kikao cha asubuhi,kushoto Mhe.Machano Othman (Muembemakumbi) na Mhe.Ali Abdalla(Mfenesini).wakitoka katika ukumbi wa mkutano.
Kushoto Mhe. Mahmoud Mohammed Mussa (Kikwajuni) na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Ramadhan Abdalla Shabani, wakibadilishana mawazo wlipokuwa wakitoka Ukumbi wa Mkutano.
Mhe. Ali Mzee, na Mhe. Nassor Mazrui (Mtoni)wakijadili jambo wakitoka Ukumbi wa Mkutano baada ya Kikao cha asubuhi.
Mhe. Ali Mzee, akisisitija jambo na Mwanasheria Mkuu wa Sherikali Zanzibar Othman Masoud,(katikati) na Mhe Ismail Jussa (Mjimkongwe) wakiwa nje ya jengo la baraza baada ya kuahirishwa kikao cha asubuhi katika
Kwa kweli vingi kati ya vikao vya baraza letu la wawakilishi havina tija!
ReplyDeleteMengi kati ya mambo wanayojadili sio ya vipaombele.
Sijui tena huo mswaada unaoendelea kujadiliwa utaleta mabadiliko gani kuhusu hizo ajira manake kuna degree 1500 hazina ajira!