Habari za Punde

Maonesho ya Asasi za Kiraia katika Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani.


 Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Kikwajuni Mhe.Mahmoud Mohammed Mussa, akikata utepe kuashiria kuzinduwa maonesho kwa Ajili ya Wajumbe wa Baraza yanayofanyika katika viwanja vya Baraza Chukwani Zanzibar. 
 Mhe.Mahmoud Mohammed Mussa, akimsikiliza Mjumbe wa Jumuiya ya Pemba Association for Civil Soceit(ZASCO)Mohammed Ussi, akitowa maelezo ya Jumuiya yao, wakati wa uzinduzi wa kazi za Jumuiya zisizo za Kiserekali.  
 Mjumbe wa Jumuiya ya Skuli za Maandalizi Madrasa (ZPMO) Mwanasama Abdalla, akitowa maelezo ya jumuiya yao jinsi inavyotoa Elimu kwa Watoto wadogo,katika madrasa mbalimbali vijiji.wakati wa maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani. 
Wanajumuiya wakishirika katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi katika maonesho ya jumuiya zao kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. kujionea jinsi vikundi vya Jumiya vinavyofanmya kazi katika majimbo yao na kujiendeleza kiuchumi.
Bango la Jumuiya ya ZIADA likitowa Ujumbe huo katika viwanja vya maonesho ya Asasi za Kiraia yanayofanyika katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi. yaliozinduliwa leo. 
Mjumbe kutoka Jumuiya ya Kuwaendeleza Watoto wa Kike Zanzibar FAWE, Arafa Kipevu, akitowa takimu za kuonesha jinsi ya Watoto wa Kike, katika maskuli mbalimbali maendeleo yao katika elimu wakati Mhe. Mahmoud alipotembelea baadhi ya mabanda ya maonesho hayo.

 Mhe Mahmoud Mohammed Mussa, akimsikiliza Mjumbe wa banda la kutowa Elimu ya Athari za  Matumizi ya Dawa za kulevya kutoka kwa Tatu Ali Faki. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.