Habari za Punde

Wafanyabiashara Eneo la Skuli ya Vikokotoni Wahamishwa

 Wafanyabiashara darajani Vikokotoni wakiondoa mabati baada ya kuamriwa na Baraza la Manispaa  kuondoa biashara zao katika eneo hilo mbele ya Skuli ya Vikokotoni.
 Eneo la mbele ya Skuli ya Vikokotoni likiwa limesafishwa baada ya kutolewa amri ya kuhama kwa Wafanyabiashara hao ili kupisha nafasi hiyo kwa ajili ya Wanafunzi na kazi nyengine za kuimarisha eneo hilo.
Wafanyabiashara wa Jua Kali wakiwa wamepingwa na butwaa  kuona eneo lao likiwa safi na kuamriwa kuondoka katika eneo hilo kufanya biashara mbele ya skuli ya Vikokotoni, awali Wafanyabiashara w Jua Kali tayari walikuwa wameshahamishiwa eneo la Saateni ilio kufanyiabiashra . Lakini bado wamekuwa wakifanya biashara zao katika eneo hilo na kuwa bughudha kwa Wanafunzi wa Skuli ya Vikokotoni wakiwa  madarasani na wakati wa kiingia skuli na kutoka kunakuwa na msongamano wa bidhaa katika eneo hilo.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.