Makamu WA Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea Maktaba ya kumbu kumbu ya Waumini wa Madhehebu ya Jews Nchini Israel iliyopo katika Mji wa Jerusalem akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Maktaba hiyo Dr. Robert Rozatt.
Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia moja ya ramani ya eneo la makaazi ya waumini wa Madhehebu ya Jews Mjini Jerusalem ambayo yaliwahi kuvamiwa na Majeshi ya Adof Hitler.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo wa Israel Bibi Orit Nokel. Kushoto yake ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi , Balozi wa Israel Nairobi na Dar es salaam Bw. Kasbia Nuriel.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Balozi Mdogo wa Tanzania Misri na Israel Bwana Jestus Nyamanga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohd pamoja na Balozi Mdogo wa Tanzania Nchini Misri na Israel Bwana Jestus Nyamanga wakiwa katika picha ya pamoja Mjini Jesrusalem.
Nyuma yao ni Msikiti mkongwe wenye Historia ndefu katika Uislamu ambao Kiongozi wa Uislamu Mtume Muhammad { SAW } alipandishwa mbinguni ndani ya usiku mmoja wa Masjid Al Aqsar.
Serikali ya Israel imekubali kuisaidia Zanzibar katika Sekta ya Kilimo ambayo bado inaendelea kuwa muhimili mkubwa wa uchumi wake .
Waziri wa Kilimo wa Israel Bibi Orit Nokel alieleza hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye yuko katika Ziara ya Kiserikali ya Siku tatu Nchini Israel. Mazungumzo ya Viongozi hao ambayo pia yalijumiisha Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed pamoja na Maofisa wa pande hizo mbili yalifanyika katika Hoteli Maarufu ndani ya Mji wa Jerusalem ya King David.
Waziri Orit alisema hatua ya kwanza imelenga kwa Wataalamu wa Ufugaji kutoka Israel wanatarajiwa kuwasili Zanzibar mwishoni mwa mwezi huu wa Mei kwa ajili ya kutoa Mafunzo kwa Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa.
Waziri huyo wa Kilimo wa Israel alifahamisha kwamba Nchi Hiyo tayai inaongoza Duniani katika masuala ya Utaalamu wa Kilimo ambao imekuwa ikiutawanya kufuatia Maonyesho ya Kilimo yanayofanyika Mwezi Mei kila Mwaka na kualikwa Nchi zipatazo 30 Duniani.
Bibi Orit Nokel ameushauri Uongozi wa Serikali ya Tanzania na Zanzibar kwa ujumla kuandaa utaratibu wa namna ya kushiriki Maonyesho hayo. Hata hivyo Waziri Orit alisema ipo haja kwa Zanzibar hivi sasa kuangalia Meneo muhimu zaidi ya kilimo ambayo Israel itakuwa tayari kuwaunga mkono kwa kusaidia Taaluma ya Kisasa zaidi.
Akitoa Shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi bado aliiomba Israel itumie uwezo wake katika kusaidia Sekta hiyo muhimu ya Kilimo. Balozi Seif alisema Zanzibar inaendelea kukabiliwa na ukosefu wa mvua za mara kwa mara hali ambayo Israel inaweza kuchangia Taaluma katika kukabiliana nayo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alilishukuru shirika la Maendeleo ya Misaada la Israel { Mashav } kwa jitihada zake za kuwafundisha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Zanzibar mbinu za Kisaa za usindikizaji wa Maziwa.
Balozi Seif na Ujumbe wake walipta fursa ya kuangalia kumbu kumbu za Waumini wa Madhehebu ya Jews katika Maktaba ya Yad Vashen ambapo zaidi ya Waumini Milioni syta wa Madhehebu hayo waliuawa katika Vita vya Pili vya Dunia.
Wakati wa Jioni Balozi Seif alitembelea Mji wa Kihistoria wa Jerusalem ikiwemo sehemu maarufu ya ukuta Mkubwa uliotenganisha Waumini wa Dini ya Kikristo na Kiislamu hapo Masjid Al Aqsa.
Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment