Joseph Ngilisho, ARUSHA
MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari amewasihi vijana jimboni humo kuachana na starehe zisizo za msingi hasa unywaji wa pombe kupindukia aina ya viroba.
Nasari aliwaeleza vijana kuwa huu ni wakati wa uwajibikaji kwa kila mtu kutumia muda kwa kufanyakazi hatua ambayo itasaidia kuinua maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla
.
Mbunge huyo alisema hayo katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha watoto yatima cha ‘African Orphanage’ kilichopo Sakila, uzinduzi ambao ulikwenda hafla ya kumuaga mwinjilishaji mkuu na mwasisi wa makanisa ya Pentekoste wilayani Arumeru, Askofu Nickson Issangya.
Alisema unywaji viroba kupindukia ni msingi ambao hauelekei kuwa na msingi wa maendeleo ya vijana na kuwataka wabuni mbinu za kufanyakazi na kuachana na utegemezi.
Aidha alisisitiza kwa wananchi katika jimbo hilo kushikamana kwa pamoja na kusahau itikadi zao za kisiasa kwani muda wa kampeni umeisha na Mbunge amepatikana.
Alisema wakazi wa jimbo hilo wengi wao wamejengeana chuki zinazosababishwa na tofauti za kisiasa hadi makanisani bila kutambua kuwa uchaguzi umekwisha na kinachotakiwa ni kuwajibika kwafanyakazi za kuleta maendeleo.
Katika hatua nyingine mbunge huyo alitoa ushuhuda wa maisha yake na kudai kuwa wakati akisoma skuli ya msingi alikuwa akiuza kwa kutembeza minadani mifuko ya plasitiki ya Marliboro, kutokana na wazazi wake kutokuwa na uwezo wa kumlipia ada.
Alisema kuwa wakati akisoma alipandikizwa maono ya ubunge na Mwenyezi Mungu, hivyo katika kipindi chote cha masomo yake kuanzia skuli ya msingi hadi Chuo Kikuu, ndoto zilizokuwa zikimjia usingizini ni kuhusua yeye kuwa Mbunge.
Aliwataka wananchi katika jimbo hilo kushikana katika kuliletea maendeleo jimbo hilo, lenye changamoto nyingi ikiwemo ya uhaba wa ardhi na kudai kuwa atafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha analeta mabadiliko na kwamba hawatajuta kumchagua.
Kwa upande wa Askofu Nickson Issangya aliwaomba wakazi wa jimboni humo kuacha kubaguana kwa itikadi za kisiasa hadi makanisani na kuwataka kupigania maendeleo yao wenyewe wakimtumaini Mwenyezi Mungu kwa kuwa kampeni za uchaguzi zimeisha na Mbunge amepatikana.
Katika hafla hiyo asari aliahidi kusaidia vituo vyote vya watoto yatima vilivyomo katika jimbo hilo na kuwataka wananchi kujikita zaidi kutoa msaada kwenye makundi yasiyojiweza hasa watoto yatima, wajane na akinamama wazee.
Kama vijana hawakunywa pombe watakuwa vipi wanachama wa CHADEMA. Nafikiri pombe ndio inayosababisha vijana hao kujiunga na chama hicho.
ReplyDeleteKwanini iwe suala la kukemea,wakati timu ya taifa ya mpira wa miguu ndio kioo chao hao vijana.ikiwa cha mpira na wizara imehalalisha kuwa pombe ndio kinywaji cha wacheza mpira kwa kuwafadhili 10million us$,
ReplyDeleteSasa kwa nn mbuge awalaaumu hao vijana,ikiwa wameamrishwa na wizara ya michezo kwa tamaa ya hizo pesa.wanafadhiliwa na mafao ya pombe.
Huyu nassari bure kabisa!!
ReplyDeleteInaonekana baada ya 'kuchemka' kwa kufichua siri ya kuunda taifa la kanda ya kaskazini ya TZA kabla ya wakati wake, sasa anataka watu wasahau kwa kuanza kampeni ya kuataza ponbe kwa vijana.