Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni, Utalii na Michezo, alipofanya ziara kutembelea eneo la Bungi linalofungw Mnara wa kurushia matangazo ya redio Bungi.
Katibu Mkuu wa Wizara Habari Zanzibar Ali Mwinyikai, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohemed Shein, alipotembelea Bungi kituo cha kurushia matangozo ya Redio Zanzibar.kulia kwa Katibu Mkuu Waziri wa Habari Utamaduni Utaliina Michezo Said Ali Mbarouk.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Fundi Mkuu wa Ujenzi wa Mnara wa Redio Steven Makange, akitowa maelezo ya ufungaji wa mnara huo huko Bungi Zanzibar.
Madarasa ya Skuli ya Unguja Ukuu yakiwa yamefanyiwa Ukarabati mkubwa na Wazanzibar wanaoishi nchini Canada, wakiwemo miongoni mwao wakiwa wamesoma katika Skuli hii miaka ya nyuma na sasa wanaishi Nchi za nje, wakisaidia miradi ya maendeleo ya Nchi yao. katika sekta mbalimbali Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Unguja ukuu, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar, maendeleo ya Ujenzi huo unaotolewa na Wananchi wa Zanzibar wanaoishi nje ya Zanzibar ikiwa ni msaada wao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha UngujaUkuu baada ya kufunguwa kituo cha Afya na kuangalia maendeleo ya Ukarabati wa Ujenzi wa madarsa matano ya skuli hiyo yanayojengwa na Wazanzibar wanaoishi nchini Canada.
Dk. Feroz Jaffarji, ni mmoja wa Wanafunzi waliosoma katika Skuli ya UngujaUkuu, ambaye anaishi Nchini Canada akitowa salamu kwa niaba ya Wazanzibar wanaoishi Canada kwa Rais wa Zanzibar kwa mchango wao kuendeleza maendeleo ya Zanzibar katika sekta za Elimu na Afya, na kuwa pamoja nae kutowa misaada kujenga nchi yao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akiangalia picha ya Wanafunzi waliosoma katika Skuli ya Lumumba katika miaka ya 60.baada ya kukabidhiwa na Dk. Feroz Jaffarji ambaye na yeye yumu katika picha hiyo wakati wakiwa Wanafunzi wa Skuli hiyo na wengi wengine wako nje ya nchi na Zanzibar.
Baadhi ya Wazanzibar wanaoishi nje ya Nchi wakiwa katika Viwanja vya Skuli ya UngujaUkuu.
Wanafunzi wa Skuli ya UngujaUkuu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar akitowa nasaha zake baada ya kutembelea ujenzi wa skuli yao unaojengwa na Wazanzibar wanaoishi nchini Canada.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa Jimbo la Uzini alipofanya ziara kutembelea bonde la Mpunga la Uzini, kuangalia maendeleo ya Kilimo hicho katika Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Afan Othman, akitowa maelezo ya ukukila wa uwangiliaji maji katika bonde hilo likiwa na wakulima 138, wakilima kilimo cha mpunga na mbogamboga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakulima wa Bonde la Uzini, wakati alipofanya ziara katika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Wakulima wa Bonde la Uzini wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alipokuwa akiwahutubia alipowatembelea kuona maendeleo ya kilimo cha mpunga bondeni hapo.
afadhali ya muwekezaji huyu kafanya la maana , kujenga na kutoa vifaa vya afya , na pia hawa wazalendo waloko Kanada kwa kuikarabati hii skuli....hivyi ndo inavyotakiwa , sisi wazenji wenyewe ndio wajenzi wa nchi yetu ...serikali ipo ipo tu
ReplyDelete