Habari za Punde

Siku tatu za maombolezo ya Saitoti


NAIROBI,Kenya

KENYA imetangaza siku tatu za maombolezi baada ya kifo cha Waziri wa Usalama wa Ndani, Profesa George Saitoti, na naibu wake, Orwa Ojode, kwenye ajali ya helikopta ya polisi katika eneo la Ngong, nje ya Nairobi.

Rais Mwai Kibaki alisema kifo cha Prof. Saitoti ni msiba mkubwa kwa taifa, na serikali imetangaza kuwa baraza la mawaziri litakutana Jumatatu (jana), kujadili tukio hilo.

Idara ya polisi imesema uchunguzi utafanywa kujua sababu ya ajali hiyo, na balozi wa Marekani mjini Nairobi, amesema Marekani iko tayari kusaidia kwenye uchunguzi huo, ikiwa itatakiwa kufanya hivo.

Msemaji wa polisi alieleza kwamba inavyoelekea kuanguka kwa helikopta hiyo lilikuwa tukio la ajali.

Raia wa Kenya walikuwa na masikitiko Jumapili, baada ya taarifa ya ajali hiyo kujulikana, na watu wamekuwa wakizuru nyumba ya kuhifadhi maiti mjini Nairobi kutoa heshima zao.

Makamu wa rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka, alipofika kwenye tukio la ajali alitoa rambi-rambi zake na alieleza wale waliokuwamo ndani ya ndege ambao wote wameteketea.

Ndege hiyo ya aina ya Eurocopter ya polisi, ambayo ilikuwa inaelekea Yugis, ilikuwa imembeba Waziri Saitoti, naibu waziri, Ojode na maafisa rubani wa ndege, Nancy Gitwanja na Luke Oyugi, na vilevile askari wawili ambao wanakuwa wanaandamana na Waziri Saitoti, Inspekta Tonkei na Thomas Murimi.

Rambirambi zimekuwa zikimiminika nchini Kenya kutoka pembe mbali mbali duniani.

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa na mpatanishi wa mgogoro wa Kenya,Kofi Annan, alisema kifo cha Saitoti ni pigo kubwa kwa siasa za Kenya.

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, ambaye alipatanisha baada ya ghasia za uchaguzi uliopita nchini kenya.

Saitoti aliwahi kuwa Makamu wa rais na waziri wa fedha katika serikali ya Rais Moi, na akitarajiwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Alifariki akiwa na umri wa miaka 67. (BBC News).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.