Zanzibar
ni nchi ya ajabu sana. Ina historia nyingi pekee kama nchi ya kwanza Afrika
kuwa na Televisheni ya rangi. Zanzibar
ni nchi pekee Afrika yenye historia ya kimaajabu kwa kutokuwa na mdudu mbaya anayeitwa Rushwa.
Kuna
Rais mmoja mstaafu aliwahi kunukuliwa akisema kwamba Zanzibar hakuna rushwa
ndiyo maana hatuna haja ya kuwepo chombo kama Takukuru.
Hili
ni mojawapo katika maajabu ya Zanzibar kuwa ni nchi pekee duniani ambayo haina
rushwa.
Kwa
nini hakuna Rushwa?
Kwasababu
hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la
rushwa.
Kwa
sababu hata akifikishwa mahakamani hakuna hiyo sheria ya rushwa ambayo itaweza
kumshitaki na hatimaye mtuhumiwa kutiwa hatiani.
Kwa
sababu Baraza letu la kutunga Sheria ( Baraza la Wawakilishi) limeipiga danadana sheria ya Rushwa miaka
dahari na kila ikiletwa Barazani hurudishwa kwa watunga Sheria waifanyie
ukarabati iwe “imara” zaidi.
Kwasababu
ukitajirika haraka haraka Zanzibar hakuna atakaehoji utajiri wako bali wako
wengi watakaosifu ujanja nausmati wako.
Kwa
sababu hatusikii viongozi wakuu wa serikali, masheikh, mapadri kuikemea rushwa kwa nguvu zote kwakuwa haipo.
Kwasababu
anayekula rushwa huwa hana huruma na wenzao anajijali yeye mwenyewe tu na
Wazanzibari ni watu wenye huruma sana na wenzao.
Kwasababu
wazanzibari wengi ni waislamu ambao hufuata misingi ya dini yao inayowakataza
kujiingiza katika vitendo vya rushwa.
Ntashindwa
kuendelea ila bora nianze kujipanga nikaanze maisha yangu katika visiwa vya Zanzibar ambavyo ni vya kimaajabu katika
dunia yetu ya leo.
Ningelipendekeza
katika kuenzi maajabu haya, Uwanja wa ndege na bandarini liwekwe Bango kubwa
linalosema “Karibu Zanzibar nchi
isiyokuwa na Rushwa”
No comments:
Post a Comment