Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akimwongoza Mtaalamu wa historia na Mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar, Profesa Abdull Sheriff kuingia katika ukumbi wa mikutano wa Tume hiyo kwa ajili ya kubadilishana mawazo na wajumbe wa Tume hiyo leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012)
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilko ya Katiba Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba (kulia) akizungumza na wajumbe wa Tume hiyo katika ofisi za Tume jiji Dar es Salaam wakati walipokuwa wakibadilishana mawazo na Mtaalamu wa historia na Mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar Profesa Abdull Sheriff (katikati) leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012). Kushoto ni Mjumbe wa Tume hiyo, Dkt. Salim Ahmed Salim
Mtaalamu wa historia na mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar, Profesa Abdul Sheriff (kushoto) akifafanua jambo katika mkutano wa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam (Jumatatu, Agosti 13, 2012). Wengine ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Joseph Warioba, Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid (kulia)
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Humphery Polepole akiongea katika mkutano kati ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mwanasheria na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Bw. Jenerali Ulimwengu. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012)
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Suleiman Omary Ali akiongea katika mkutano kati ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mwanasheria na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Bw. Jenerali Ulimwengu. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012).
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Joseph Butiku (kulia) na Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) wakibadilishana mawazo na Naibu Katibu wa Tume hiyo Bw. Casmir Kyuki katika mkutano kati ya Wajumbe wa Tume hiyo na Mtaalam wa Historia na Mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar, Prof. Abdul Sheriff. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012)
Picha zote na Tume ya Katiba
Na Mwandishi Wetu
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameendelea kukutana na kubadilishana mawazo na uzoefu na Wataalam mbalimbali kuhusu Katiba Mpya kwa lengo la kuongeza uelewa wao na leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012), kwa nyakati tofauti, Wajumbe wamekutana na Prof. Abdul Sheriff na Ndg. Jenerali Ulimwengu.
Tayari Tume hiyo imeshawaalika na kukutana na kwa nyakati tofauti na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza mzalendo Jaji Mark Bomani, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Pius Msekwa na Mhadhiri wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa Shivji.
Prof. Sheriff ni mtaalam wa historia na mwanaharakati wa siku nyingi kutoka Zanzibar na kwa muda mrefu amekuwa akishiriki na kutoa mada katika makongamano mbalimbali yanayohusu Katiba.
Ndg.Ulimwengu ni Mwanasheria na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi ambaye pia ameshiriki na kutoa mada katika makongamano mbalimbali yanayohusu Katiba Mpya.
Akizungumza wakati akiwakaribisha, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatambua kuwa Tanzania ina wataalam wanaoweza kutoa mchango mkubwa katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba na kuwasihi wanapopata nafasi wasisite kuwasilisha maoni yao kwa Tume.
“Tukipata nafasi, huwa tunawaomba wataalam kama ninyi kuja kubadilishana mawazo na Wajumbe wa Tume. Ni matumaini yangu kuwa Wajumbe wa Tume watafaidika sana na utaalam wako katika kupanua mawazo,” alisema Jaji Warioba katika mkutano uliohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhani, Wajumbe wengine wa Tume na Sekretarieti ya Tume.
Jaji Warioba aliongeza kuwa Tume imejiwekea utaratibu wa kukutana na makundi mengine mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kubadilishana mawazo na kupokea maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Akiongea katika mkutano huo leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012), Prof. Sheriff pamoja na kushukuru kwa kualikwa na Tume, alizungumzia uzoefu wake katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba unaoendelea na kutoa maoni yake katika masuala mbalimbali yakiwemo Muungano na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Kwa upande wake, Ndg. Ulimwengu ambaye amekutana na Tume hiyo leo (Jumatatu, Agosti 13, 2012) mchana, pamoja na mambo mengine, alizungumzia umuhimu wa kuandika Katiba Mpya itakayotumiwa na Watanzania kwa miaka mingi ijayo katika kuwaletea maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.
maoni yetu kwenu ni kwamba hatutaki muungano , kwa hio suala la katiba lifungiliwe mbali warudi walikotoka , Ndugu yetu Asaa , jukumu la kuwa ktk kamati hii ulijue na huenda ikawa bora kwako kujiuzulu kabla hujatumiwa kuwauza ndugu zako waznz , simtaji salimu hemedi salimu kwa sababu yeye ni mjukuu wa nyerere , aliwauza wenzake kwa manufaa kidogo ya kilimwengu , na sasa hayuko mbali na kukutana na Mola, umri aliobakisha duniani ni mdogo kuliko wa kukutana na Muumba , lakini bado dunia imemzonga , WANZANZIBARI HAWATAKI MUUNGANO
ReplyDelete