Taasisi mbalimbali za kidini hapa nchini zilizopata usajili rasmi kwa Mrajis Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekanusha kuhusika na tamko lililotolewa na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mselem Ali la Waislamu wa Zanzibar wagomee kushiriki katika Sensa ya Watu na Makaazi Kitaifa inayotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.
Wakizungumza na Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga Wawakilishi wa Taasisi hizo wamelaani tabia ya Uamsho ya kujipa Mamlaka ya kuzisemea Taasisi hizo.
Aidha,wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuthibitisha ni kikao gani kilichokaa na kuzungumza na Taasisi za Kidini na kuamua kwa pamoja kutowa tamko hilo la kupinga kushiriki kwa Waislamu katika Sensa.
Aidha, wameihakikishia Afisi ya Mufti na Serikali kuwa watashiriki katika Sensa ili kusaidia maendeleo ya Zanzibar na kutatua baadhi ya migogoro ya kijamii na sio kujiingiza katika siasa na kupingana na Serikali kama ambavyo imekuwa ikifanya Jumuiya ya Uamsho.
Taasisi zimewataka Waislamu kushirikiana na Serikali na kuachana upotoshaji unaofanywa na Uamsho.
Aidha, wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuachana mara moja kutumia kivuli cha umoja wa Taasisi za kidini Zanzibar wanapoamua mambo yao kwani Jumuiya hizo nyingi hazikubaliani na Sera yao ya fujo na vurugu.
Mwisho.
Imetolewa na:
Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzibar
Hebu twambieni basi hizo taasisi ni zipi na hicho kikao kilifanyika lini.Sote tunajua kuwa Fadhil Soraga ni kimbele mbele na yuko tayari jina lake kutumika kukidhi matakwa ya serikali.Ukweli ni kwamba Serikali imeshindwa kujibu hoja za Uamsho.Vipi leo unaninyima kipande cha mzanzibari ambacho ni haki yangu kisheria lakini wakati huo huo unanitaka nihesabiwe.
ReplyDeleteWASALITI WANAYOIKUBALI SENSA-WAJITOKEZA.
ReplyDeleteBaadhi ya vyombo vya habari vikiwemo vya Serikali jana walitoa taarifa kwa kudai ati baadhi ya Taasisi za kislamu zilizoungana katika harakati za ukombozi wa Zanzibar zimesema hazikushirikishwa katika swala la sensa ya watu na makaazi inayotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili..
Taasisi zilizoungana na kuwa kitu kimoja ni jumla ya Taasisi za Kiislamu 32 na zote zimeshiriki katika vikao vyote vya upingaji sensa tunavitaka vyombo hivo ikiwemo Zenji fm, Radio Zanzibr na Zbc viache kupotosha umma.
Vile vile zimejitokeza baadhi ya Taasisi za kiislamu ambazo hazimo katika 32 wameanza kuwasaliti Waislamu kwa maslahi yao binafsi na kwa kuiogopa Serikali. .
Taasisi hizo ni ya Tahfidhul Qur'aan inayongozwa na Maalim Sule ya Kikwajuni na Jumuiya ya Mahdu Juneid inayongozwa na Ust Samir hawa wanaungana na Bakwata na Ofisi ya Mufti na wamewahamasisha wanachama wao na wafuasi wao washiriki sensa.
LAKINI SISI HATURUDI NYUMA KAMA WAO WATASHIRIKI SISI MSIMAMO WETU UKO PALE PALE HATATAKI SENSA.
Tunataka nchi yetu Sensa baadae.