
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe akisoma risala kumkaribisha Makamu wa kwanza wa Rais

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, akiweka saini kwenye Kitabu cha Wageni kwenye Ofisi wa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi hizo za Ubalozi. Pichani: Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, akishuhudia uwekaji wa saini, mara baada ya kumkaribisha Ofisini hapo

Makamu
wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza, Mheshimiwa. Peter Kallaghe, wakiwa kwenye Picha ya pamoja na
Maafisa wa Ubalozi, Wajumbe na Wawakilishi kutoka Serikali ya
Zanzibar
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliwasili
London, Uingereza juzi usiku (Jumanne, 11 Septemba 2012) kwa ziara ya siku nne
akitokea Marekani alikokwenda kuhudhuria Mkutano wa Democratic Party, kwa
mwaliko rasmi wa chama hicho. Maalim Seif jana (Jumatano, 12 Septemba 2012)
alitembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo hapa London na kuzungumza na Maafisa wa
Ubalozi huo na baadae kula nao chakula cha mchana. Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar leo asubuhi amekutana na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Uingereza,
Mheshimiwa Mark Simmonds na mchana huu anakutana na mabalozi wa nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki waliopo hapa London. Kesho Mheshimiwa Maalim Seif
anatarajiwa kukutana na Watanzania wote walioko London katika sehemu
itakayotangazwa hapo baadae, kabla ya kuanza safari ya kurejea Tanzania Jumamosi
asubuhi.
Picha na habariMr. A. Rashid Dilunga
ICT - Manager
Tanzania High Commission
Tanzania Trade Centre
3 Stratford Place
London W1C 1AS
Tel: +44(0) 207 758 8070
Fax: +44(0) 207 758 8073
Email: dilunga@tanzatrade.co.uk
Web: tanzatrade.co.uk
Picha na habariMr. A. Rashid Dilunga
ICT - Manager
Tanzania High Commission
Tanzania Trade Centre
3 Stratford Place
London W1C 1AS
Tel: +44(0) 207 758 8070
Fax: +44(0) 207 758 8073
Email: dilunga@tanzatrade.co.uk
Web: tanzatrade.co.uk
No comments:
Post a Comment