Habari za Punde

Mnara wa Zantel karibu na uwanja wa ndege wa Karume Pemba walalamikiwa

 
KAMATI ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mwakilishi wa la Jimbo la Kojani Hassan Hamad Omar mwenye suti kushoto akitoa maelezo baada ya kupewa taarifa ya ujenzi ya ujenzi mnara wa kampuni ya simu ya Zantel, kutoka kwa Meneja wa wa Uwanja wa Ndege Pemba Amour Mussa kulia, katika Kijiji cha Furaha karibu na uwanja wa ndege wa Karume Pemba, ambapo ujenzi huo ulitolewa kibali na Mamlaka ya Mawasiliano ya Anga Tanzania (TCAA) umetajwa kuwa unaweza kusababisha athari wakati wa kutua na kuruka kwa ndege. (picha na Haji Nassor, Pemba)


Mafundi ambao hawakupatikana majina yao, wakiwa katika harakati za ujenzi wa mnara wa kampuni ya simu ya mkononi ya Zantel huko kijiji cha Furaha Wilaya ya Chake chake mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Karume Pemba, ambapo ujenzi huo unalalamikiwa vikali na uongozi wa uwanja wa ndege na ‘mapilot’ wakisema unaweza kuleta athari wakati wa utuwaji na urukaji wa ndege (picha na Haji Nassor, Pemba)  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.