Makamuwa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Naibu Waziriwa Mambo ya nje wa Uingereza anayeshughulikia masuali ya Jumuiya ya Madola bwana Mark Simmonds, katika ofisi za Wizara hiyo mjini London.
Makamuwa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na maveterani wa Uingereza walipokutana mjini London jana tarehe 14/09/2012
Na, Mwandishi Maalum, London
Makamu wa Kwanza wa Rais wa ZanzibarMaalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar yenye muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa inafanyakazi zake vizuri na inakaribisha wawekezaji kutoka sehemu mbali mbali dunianikwa lengo la kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi.
Amesema viongozi wa serikali hiyo kutoka vyama vya CCM na CUF wamekuwa wakishirikiana vyema na wananchi katika jitihadaza kuendeleza umoja wa kitaifa ambao ulitokewa kwa kipindi kirefu.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo mjini London Uingereza, alipokuwa akijibu masuali mbali mbali kutoka kwa mabalozi wa nchiza Afrika pamoja na maveterani wa Uingereza, waliokutana kuzungumzia masuala mbali mbali yanayohusu maendeleo ya Zanzibar.
Katika masuala yao ya msingi, mabalozi na maveterani hao walitaka kujua juu ya mustakbali wa Zanzibar pamoja na maendeleoya serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka2010.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema licha ya changamoto ndogo ndogo zilizopo kutoka kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa ngazi za chini, Serikali ya Umoja wa kitaifa imepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kurejesha umoja wa Wazanzibari pamoja na kuweka mazingira bora ya kuvutia wawekezaji.
Kabla ya mkutano huo wa mabalozi, MaalimSeif amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza anayeshughulikia masuali ya Jumuiya ya Madola bwana Mark Simmonds, katika ofisi za Wizarahiyo mjini London.
Katika hatua nyengine Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amekutana na baadhi ya viongozi wa Umoja wa WazanzibariWanaoishi Uingereza Zanzibar WalfareAssociation (ZAWA) na kubadilishana mawazo juu ya mambo mbali mbali yanayoihusu zanzibar ikiwa ni pamoja na kuimarisha idara ya Diaspora, ili iweze kuwa karibu zaidi na wazanzibari wanaoishi nchi za nje.
Viongozi wa jumuiya hiyo wametaja mafanikio mbali mbali yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na kuanzisha asasi za kijamii nchii Uingereza ambazo zitawaunganisha wazanzibariwanaoishi nchini humo.
Jumuiya hiyo pia imeelezea nia yake yakuleta maendeleo Zanzibar kupitia jitihada mbali
mbali ikiwa ni pamoja nakujjipanga katika kusaidia vifaa na vitendea kazi zikiwemo kompyuta.
Kwa upande wake Maalim Seif aliwasisitiza Wazanzibari wanaoishi nchini Uingereza na kuwataka kuendeleza umoja na mshikamano wanapokuwa nje ya nchi, sambamba na kufikiria namna wanavyoweza kuisaidia nchi yao kimaendeleo.
Maalim Seif aliwasili nchini Uingerezatarehe 12 Septemba 2012, baada ya kumaliza ziara yake nchini Marekani, ambapomara tu baada ya kuwasili alitembelea ofisi za ubalozi wa Tanzania mjini London kwa lengo la kusalimiana na wafanyakazi wa ubalozi huo.
No comments:
Post a Comment