Habari za Punde

Balozi Seif afungua mkutano wa Jumuiya ya wazazi ya CCM mkoa wa kaskazini Unguja

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Kaskazini Unguja Hapo Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope uliopo Kinduni . Kulia ya Balozi ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja ambae pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Tanzania Zanzibar Nd. Mussa Ame Silima na Kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa Kaskazini Unguja Bibi Caterine Peter Nao
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja Hapo Ukumbi wa CCM Jimbo la Kitope uliopo Kinduni
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatialia Hotuba ya Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo Balozi Seif Ali Iddi ambae ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM hapo kinduni Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope.
 
 
Na Othman Khamis Ame , OMPR
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema sifa sahihi watakayoendelea kupewa Wazazi popote pale itapatikana endapo jukumu la kuwalea Watoto wao watalipa kipaumbele kinachostahiki.
Balozi Seif ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba mfumo wa utandawazi wa Dunia uliopo hivi sasa umechangia kuathiri malezi bora ya Vijana ndani ya Jamii licha ya kwamba upande mmoja unaelimisha.
Akiufungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja hapo ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope Balozi Seif alisema Jumuiya hiyo hivi sasa ina kazi nzito ya malezi ya Vijana kutokana na mfumo huo wa Utandawazi.
Balozi Seif alionya kwamba baadhi ya Wazazi Nchini wanahusika katika janga la upotofu wa maadili kwa Vijana kutokana na kuwaridhia Watoto wao kupindukia na matokeo yake Watoto hao kukosa Heshima kwa kiwango cha kutisha.
“ Utandawazi kwa kiasi kikubwa umeharibu mfumo wa malezi na kupelekea baadhi ya watoto kuwaita Baba zao Madingi wakati Mama wakiwaita Mom. Sasa tunakwenaa wapi?”. Aliuliza Balozi Seif Ali Iddi.
“ U dot. Com wao walioubeba Vijana hvivi sasa unawaharibia maadili yao. Sasa watoto wetu Heshima zao zimepungua kutokana na utandawazi ulituharibia mfumo wetu wa malezi”. Alieleza Balozi Seif Ali Iddi.
Alisema Wanajumuiya hiyo ya Wazazi lazima wawadhihirishie Wananchi, CCM na Vijana wote kwamba Jumuiya hiyo ina nguvu kwa vile inabeba watu wa rika zote katika Jamii inayowazunguuka.
Balozi Seif amewashauri Viongozi wapya watakaochaguliwa katika Mkutano huo kukubali kubeba dhamana ya kuwa Waaminifu, Waadilifu na upendo ili kuisaidia Serikali Kuu kwa wao ndio walezi katika kutoa Elimu kwa Watoto.
“ Chagua Kiongozi unaeamini kwamba ni mahiri na madhubuti ambaye atakuwa na nguvu na ubunifu katika kuiwezesha Jumuiya bau Jamii kupata mapato yake bila ya kutegemea mwega mwengine”. Alisisitiza Balozi Seif.
Akizungumzia suala la amani Balozi Seif aliitaka Jamii kupiga vita dalili zote zinazoashiria kuvurugika kwa Amani ambayo ikitoweka hakutakuwa na wakati wa kujenga Uchumi wa Taifa.
Aliwakumbusha Viongozi wa Jumuiya hiyo ya Wazazi pamoja na Wana CCM kuendelea kuisimamia Amani iliyopo Nchini kama Ilani ya Chama hicho Ibara ya 168 ilivyoelekeza kusimia amani ya Nchi.
“ Kuna watu wanataka kutuondoshea amani yetu tuliyonayo kwa karne kadhaa zilizopita. Hili ni jukumu letu. Hivyo tunapaswa kupambana na wote wanaotaka kutuvurugia amani yetu”. Alisisitiza Balozi Seif.
Aliwakumbusha Wana CCM wote kuendelea kutetea sera na Ilani za Chama chao kwa wazi bila ya kificho kwa vile wanaziamini na walishiriki katika kuzitengeneza.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM liwapongeza Viongozi wote waliochanguliwa kuanzia ngazi ya shina hadi Wilaya na kuridhika na chaguzi hizo zilizokwenda kwa amani na utulivu.
Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja ambae pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania upande wa Zanzibar Nd. Mussa Ame Silima alisema Jumuiya ya Wazazi inaendelea kufanya chaguzi zake katika ngazi mbali mbali sambamba na Jumuiya nyengine kutokana na mabadiliko ya ngazi za juu ya CCM.
Ndugu Mussa alisema Jumuiya ya wazazi sasa italazimika kufanya chaguzi zake katika kipindi cha kila baada ya miaka mitano badala ya miaka mine iliyokuwa ikifanya hapo kabla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.