Na
Mwantanga Ame
MAMLAKA
ya vitambulisho vya Taifa Tanzania (NIDA), inatarajia kuanza zoezi la usajili
kwa wananchi wa Zanzibar
Oktoba 10 mwaka huu.
Mkugenzi
wa NIDA-Zanzibar, Vuai Mussa Vuai, aliyasema hayo jana wakati akitoa taarifa
kwa waandishi wa habari juu zoezi hilo
litavyoweza kufanyika.
Mkurugenzi
huyo alisema wananchi wote watasajiliwa
ili kupata vitambulisho hivyo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sheria
ya nchi ambayo inawataka wananchi wote kuwa na vitambulisho hivyo.
Alisema
zoezi hilo
litaanzaa kufanyika katika Mkoa wa Kusini Unguja katika wilaya Kusini ambapo litachukua kipindi cha wiki mbili
kuanzia Oktoba 15 hadi Novemba 26.
Wananchi
wa wilaya ya Kati wataanza kusajiliwa kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 9, mwaka huu na wilaya ya
Magharibi zoezi hilo
litaanza Novemba 12 hadi 23.
Wilaya
ya Mjini zoezi litaanza Novemba 26 hadi Disemba 7, mwaka huu na baadae
linatarajiwa kuhamia katika wilaya ya Kaskazini ‘B’ ambapo wananchi wa sehemu
hiyo wataanza kusajiliwa Disemba 10 hadi 21, mwaka huu na wilaya ya kaskazini
‘A’ watasajiliwa kuanzia Januari 4, 2013.
Alisema
wilaya za Pemba wananchi wataanza kuzajiliwa kuanzia Januari 7 hadi 18, mwakani
na Micheweni ni kuanzia Januari 21, hadi Febuari 2, Wete zoezi litaanza Febuari
4 hadi Febuari 15 wakati Chake Chake
litaanza Febuari 18 hadi Machi 1 mwaka huo.
Alisema
vitambulisho hivyo vinatarajiwa kutolewa kwa mfumo wa makundi matatu ambapo
utawahusisha wananchi, wageni na wakimbizi.
Alisema mtu amabaye atakuwa amehukumiwa adhabu ya
kifo, punguwani wa akili kwa mujibu wa sheria hiyo hatasajiliwa.
Alisma
katika zoezi hilo
wananchi watapaswa kutoa ushirikiano kuweza kulifanikisha na kuacha
kuwashirikisha wageni kwa njia za siri jambo amabalo likibainika wahusika
watachukuliwa hatua za kisheria.
Alisema
searikali imeamua kuanzisha zoezi hilo
kwa dhamira ya kuwatambua watu wanaoishi
nchini kwa sasa kwani kumeonekana utambuzi huo haupo jambo ambalo limekuwa
likiisababihia serikali kupata hasara.
Alisema
vitambulisho hivyo vitaweza kusaidia Bodi ya Mikopo ya Wanafuzi wa Elimu ya Juu
kuwatambua wanafunzi wanaostahili kupatiwa mikopo kutokana na hivi sasa
kuonekana kuwapo ugumu wa urudishaji mikopo hiyo.
Alisema
tatizo la kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na raia wa nchi
jirani na wafungwa waliomaliza adhabu zao au wanaoachiwa huru kwa msamaha wa rais
hivi sasa umekuwa mgumu kutokana na kushindwa kutambuliwa.
Alisema
tatizo la kuongezeka kwa mrundikano wa wafungwa katika magereza kutokana na
kutokuwapo udhibiti wa wafungwa wa kifungo cha nje nalo linahitaji kupatiwa
ufumbuzi baada ya vitambulisho hivyo vitapoanza kutumuika.
No comments:
Post a Comment