Habari za Punde

Semina ya viongozi wa Serikali kuimarisha uhusiano baina ya viongozi wa kisiasa na kiutendaji ilivyoendelea


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisisitiza jambo wakati wa Semina ya Siku tatu ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji
katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,iliyomalizika leo katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,(kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwa Mwenyekiti wa Semina ya kuimarisha uhusiano Baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,kwa siku ya tatu,semina hiyo ikiendelea
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwa Mwenyekiti wa Semina ya kuimarisha uhusiano Baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,akitoa maelekezo kwa wajumbe wakati semina hiyo ikiendelea kwa siku ya tatu,(kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
 Washauri wa Rais wa masuala mbli mbali wakiwa katika semina ya kuimarisha uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na kiutendaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,katika ukumbi wa
Zanzibar Beach Resort,wakifuatilia kwa makini mada zilizotolewa na michango mbali mbali iliyotolewa katika semina hiyo
 Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,na Watendaji Wakuu wakimsikiliza mtoa mada ya Udhibiti na Ukaguzi wa Fedha za Serikali,iliyotolewa katika semina ya kuimarisha
uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na kiutendaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort
Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali Bi Fatma akiwasililisha mada ya Udhibiti na Ukaguzi wa Fedha za Serikali katika semina ya kuimarisha uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na kiutendaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort

Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.