Habari za Punde

Wazee CCM wapongeza hotuba ya Dk. Shein


Na Mwandishi wetu

BARAZA la Ushauri la Wazee wa Chama cha Mapinduzi limempongeza Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein kwa kauli yake aliyoitoa katika hotuba ya Baraza la Idd-el-Hajj mwaka huu ya kuwanasihi wananchi wasifanye fujo na vurugu na kusema watakaofanya serikali haitawavumilia.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ,Mwenyekiti wa Baraza hilo, Makame Mzee Suleiman alisema kwa upande wao wamefarajika kusikia kauli hiyo na kwamba serikali itawatachukuliwa hatua za kisheria wale ambao walihusika katika vurugu .

Mwenyekiti huyo alisema katika hotuba hiyo Dk. Shein alieleza misimamo ya serikali kuhusu makundi ya kihalifu na anapaswa kupongezwa.

Mwenyekiti huyo alisema athari za vurugu hazichagui na humkumba aliyekuwemo na asiyekuwemo, hivyo wana imani na Dk. Shein kwa serikali yake itadhibiti hali hiyo isitokee tena.
Alifahamisha kuwa uharibifu wa barabara zilizojengwa vizuri kwa lami, kukatwa miti iliyopandwa, kuchomwa matairi mabovu na kuchafua mji kila sehemu imesebabisha kupoteza haiba ya mji wa Zanzibar.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kitendo cha kiongozi wa Umsho, Farid Hadi kujipoteza na wafuasi wake kudai anashikiliwa na vyombo vya dola ni mchezo wa kuigiza wa kutaka kumjengea umaarufu na kuiweka nchi pabaya .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.