Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (kulia) akipokea sehemu ya mchango wa nakala 100,000 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Ndg. Hebron Mwakagenda leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa Jukwaa la Katiba Bi. Diana Kilala.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba anayeshughulia utafiti Bw. Mohammed Hamad (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya Wajumbe wa Jukwaa la Katiba (kushoto) waliotembelea ofisi za Tume jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba anayeshughulikia uandaaji wa taarifa rasmi (hansard) Bi. Hanifa Masaninga (kulia) akiongea na baadhi ya Wajumbe wa Jukwaa la Katiba (kushoto) waliotembelea ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumanne, Nov. 27, 2012).
Naibu Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Casmir Kyuki (kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Jukwaa la Katiba (kulia) kuhusu uchambuzi wa maoni wakati wajumbe hao walipofanya ziara katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo
Mjumbe wa Jukwaa la Katiba Bw. Patience Sekinabo akiuliza swali kuhusu kazi ya utafiti kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba anayeshughulia utafiti Bw. Mohammed Hamad (kulia) wakati wa ziara ya iliyofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment