Habari za Punde

Waziri wa Habari Zanzibar Said Mbarouk, Akutana na Ujumbe wa Turky.

 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk, akizungumza na Ujumbe wa  Turkey  ukiongozwa na Waziri wa Kilimo na Chakula wa Turkey Mchmet Mehdi Eker kulia akiwa pamoja na Balozi wa Turkey nchini Tanzania Ali Davutoglu wakimsikiza Waziri wa Habari Utalii,Utamaduni na Michezo, walipokua wakibadilishana mawazo kuhusu kuimarisha sekta ya Utalii hapa Zanzibar, mazungumzo hayo yamefanyika katika  ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Kikwajuni leo.
 Waziri wa Habari Utalii,Utamaduni na Michezo Zanzibar Saidi Ali Mbarouk akimpa zawadi ya nembo ya visiwa vya Unguja na Pemba mgeni wake  Waziri wa Kilimo na Chakula wa Turkey Mchmet Mehdi Eker
Waziri wa Kilimo na Chakula wa Turkey Mchmet Mehdi Eker akimpa zawadi Waziri wa Habari Utalii,Utamaduni na Michezo Saidi Ali Mbarouk huko katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Kikwajuni leo

Na Ali Issa - Maelezo Zanzibar.Waziri wa kilimo na chakula kutoka Serikali ya Uturuki Mchmet Mehdí Eker ameishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupanga mikakati ya kuifanya Sekta ya Utalii kuwa na manufaa moja kwa moja kwa Wazalendo badala ya Sekta hiyo kunufaisha wageni kutoka nje ya nchi.

Hayo ameyasema leo katika ziara yake ya kumtembelea Waziri wa Habari, Utalii,Utamaduni na Michezo Zanzíbar Said Ali Mbarouk Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzíbar.

Amesema wananchi ndio warithi wakubwa wa Serikali yao ilioko madarakani hivyo hakuna budi wao kufaidika mwazo na matunda ya utalii yaliyopo kabla ya kuwanufaisha wageni kutoka nje.

Amesema hali hiyo iwapo itafikiwa vizuri wananchi watapiga hatua kubwa kimaendeleo na kuepukana na umasikini unao wakabili.

Amesema maendeleo ya Sekta ya Utalii nchini Uturuki yanawanufaisha wananchi moja kwa moja kwa kuwapa kipaumbele wao badala ya wageni jambo ambalo limeifanya nchi hiyo kupiga hatua ya kimaendeleo na kuepukana na tatizo la ukosefu wa ajira.

“sisi nchi yetu kitu cha mwazo katika sekta ya utalii ni kuona kua wananchi wetu ndio wanaofaidika zaidi na baadaye kufuata wageni”alisema Waziri huyo.

Aidha Waziri huyo ameishauri Serikali kutilia mkazo kilimo cha mazao ya matunda ambayo yataweza kukidhi mahitaji ya Watalii ambao wanakuja kutembelea Zanzíbar jambo ambalo pia litachochea ongezeko la Watalii Zanzibar.

Waziri huyo amemuomba Waziri wa Habari na Utalii nchini kuweka mkazo katika kuulinda utamaduni wa Zanzíbar ili utalii usiwe kigezo cha kuharibu tamaduni na Silka za Zanzíbar.

Waziri Mchmet alimuahidi Waziri huyo kuwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla zitafaidika zaidi kwa kupata wataalamu wa kilimo kwani Uturuki imeelekeza nguvu zake katika kuisaidia Tanzania katika Sekta ya kilimo

Kwa upande wake Waziri wa Habari utalii utamaduni na michezo Saidi Ali Mbarouk alimshukuru Waziri huyo kwa jinsi Uturuki ilivyojipanga kuisaidia Zanzíbar na Tanzania na kumuhakikishia kuwa Zanzibar itayafanyia kazi mawazo hayo hasa ikizingatiwa kuwa dhana ya “Utalii kwa wote” imeshazinduliwa ili kuwanufaisha wananchi.

Waziri Saidi alimuomba waziri huyo kuishauri nchi yake kuanzisha Safari za ndege za moja kwa moja kutoka Uturuki kuja Zanzibar na kuleta watalii wao ili kujionea vivutio vingi vya utalii vilivyopo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.