Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Amaan wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar akiongozwa na Mapikipiki.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikaguwa bwaride la sherehe za sherehe za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar
lililofanyika katika viwanja vya Amaan..
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akirudi katika jukwaa baada ya kukaguwa bwaride la sherehe za sherehe za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar
lililofanyika katika viwanja vya Amaan..
Waheshimiwa wakisoma gazeti la Zanzibar Leo lenye toleo maalum la Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 49.
Rais Mstaaf wa Zanzibar Komando Dk Salimin Amour akiwasili katika viwanja vya Amaan na kusalimiana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi Tanzania.
Rais Mstaaf wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na Mke Mama Siti Mwinyi wakiwasili katika
viwanja vya Amaan na kusalimiana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi
Tanzania.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis, alipowasili katika viwanja vya Amaan kuhudhulia sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya Amaan kuhudhuria sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika viwanja vya amaan katika sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea maandamano ya Wananchi wakiingia katika viwanja vya Amaan, kusherehe miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vijana wakiwa na picha ya Muasisi wacMapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume, wakiingia katika viwanja vya Amaan.
Askari Polisi Kikosi cha Wanawake wakipita kwa mwendo wa harakaharaka.
Kikosi cha FFU wakipita kwa mwendo wa pole.
Askari wa Kikosi cha Wanamaji KMKM wakipita kwa mwendo wa haraka haraka.
Askari wa Chuo cha Mafunzo wakitowa saluti mbele ya Mgeni Raismin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Wajajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania wakiwa katika Vyazi rasmin wakipita mbele ya Viongozi kuonesha umahiri wao katika ulinzi wa Nchi.
Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao Tanzania wakihudhuria sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment