Habari za Punde

Sherehe nusu karne ya mapinduzi kuwa za kihistoria


Na Othman Khamis, OMPR

SERIKALI inakusudia kujiandaa mapema na maandalizi makubwa ya maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kutimia miaka 50 ambazo zitatarajiwa kuwa za kihistoria.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif alitoa kauli hiyo  wakati wa tafrija maalum ya kupongezana na kuelewana kwa maafisa wa gwaride iliyofanyika hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Balozi Seif alisema ili kufanikisha azma hiyo ya serikali,mashirika, taasisi za kijamii na watu binafsi wanapaswa kuanza na maandalizi mapema kwa lengo la kupata ufanisi unaokusudiwa.

Alisema serikali itaendelea kuunga mkono vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuwa ndivyo vyenye nafasi kubwa ya kusherehesha.

Alieleza kuwa vikosi vya ulinzi na usalama vimefanya kazi kubwa mwaka huu iliyopelekea kufurahisha na kupendezesha maadhimisho hayo.
Alisema mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964  yameleta faida kubwa kwa wananchi waliowengi na kuwafanya kuwa mstari wa mbele katika maendeleo na kusherehekea sherehe hizo.
Akimkaribisha Balozi Seif, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais , Mohammed Aboud alisema majeshi ya ulinzi yameonesha umahiri mkubwa katika kuchapa gwaride.
Mapema kamanda wa Brigedi 101 Zanzibar, Brigedia Jenerali, Sharif Sheikh ameahidi vikosi vya ulinzi na usalama vitaendelea kushirikiana na serikali katika kuona maandalizi ya maadhimisho miaka 50  ya mapinduzi yanafanikiwa kwa ufanisi zaidi.

1 comment:

  1. mapinduzi gani hayo yalitoa roho za watu wasio na hatia? ndio maana mmelaaniwa mpaka leo si umeme wala maji mmeweza kusambaza ktk visiwa ukubwa wake hauzidi mkoa wowote kule bara kwa mabasha zenu , mambo muhimu yankushindeni mnafikiria kusheherekea , hospitali na shule zote mahututi , wendawazimu waliovaa kistaarabu ,

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.