Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Nchini (TAHLISO) mara baada ya viongozi hao kuwasilisha maoni ya umoja huo kuhusu Katiba Mpya kwa Tume katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Humphrey Polepole (kulia) akiongea na viongozi wa Jukwaa la Mamlaka na Taasisi zinazosimamia na kuthibiti ubora wa elimu nchini ulioongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Sifuni Mchome (kushoto). Jukwaa hilo lilikutana na Tume katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo
Mkenda akiongea - Mjumbe wa Jukwaa la Mamlaka na Taasisi zinazosimamia na kuthibiti ubora wa elimu nchini Dkt. Primus Nkwera amabye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) akitoa maoni ya jukwaa hilo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumapili, Jan 13, 2013). Kulia ni Mjumbe wa Tume Bw. Humphrey Polepole na kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Prof. Sifuni Mchome.
No comments:
Post a Comment