Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Dk. Rawya Saud Al-Busaid wakati ujumbe elimu wa Oman ulipofika ofisini kwake Migombani leo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi zawadi ya kitabu kwa Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Dk. Rawya Saud Al-Busaid baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Dk. Rawya Saud Al-Busaid nje ya ofisi yake, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migomba
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa sekta ya elimu ya juu wa Oman ukiongozwa na Waziri wake Dk. Rawya Saud Al-Busaid (wa pili kushoto), baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani. (Picha na Salmin Said, OMKR)
Maalim Seif Akutana na Waziri wa Elimu wa Oman Dk. Rawya.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesifu mchango wa Oman katika kuunga mkono sekta ya elimu nchini.
Amesema hatua hiyo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Elimu wa Sultan Qaboos, itaisaidia Zanzibar kupata wataalamu wa fani mbali mbali wanaoendana na mahitaji ya wakati uliopo wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Maalim Seif ameeleza hayo ofisini kwake Migombani alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa Wizara ya elimu ya juu ya Oman ukiongozwa na waziri wake Dk.Rawya Saud Al-Busaid.
Amesisitiza haja ya kuwepo kwa uwazi na ukweli katika hatua ya uteuzi wa wanafunzi watakaopatiwa udhamini kupitia mfuko huo wa Elimu ya juu wa Sultan Qaboos, kwa kuzingatia sifa za wanafunzi ili kupata wataalamu bora hapo baadaye.
Amesema Zanzibar kwa sasa inakabiliwa na uhaba wa walimu wa Sayansi na hisabati, jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa pia katika uteuzi huo, ili kuweza kupata wataalamu wa masomo hayo na kutatua kero hiyo ambayo ni ya muda mrefu sasa.
Ameueleza ujumbe huo kuwa Zanzibar pia inajipanga kuimarisha maktaba zake, ili kuwa na maktaba za kisasa zitakazokidhi mahitaji ya wananchi katika kujipatia taaluma mbali mbali.
Katika hatua nyengine Maalim Seif amewakaribisha wawekezaji wa Oman kuja kuwekeza Zanzibar hasa katika sekta ya utalii ambayo ni sekta muhimu kwa uchumi wa Zanzibar na upatikanaji wa fedha za kigeni.
Amesema Serikali imekusudia kuendeleza dhana ya “utalii kwa wote”, ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi ananufaika ya sekta hiyo.
Amefahamisha kuwa Oman na Zanzibar ni nchi zenye historia ndefu ya kindugu, hivyo Serikali inathamini michango inayotolewa na Oman katika kuunga mkono sekta mbali mbali za maendeleo kwa Zanzibar.
Ameelezea umuhimu wa viongozi na wananchi wa pande hizo mbili kufanya ziara za kutembeleana mara kwa mara ili kukuza uhusiano na maelewano ya muda mrefu yaliyopo baina ya Zanzibar na Oman.
Nae Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Dk.Rawya Saud Al-Busaid amesema Serikali ya Oman kupitia mfuko wa elimu ya juu wa Sultan Qaboos, inakusudia kutekeleza mpango wake wa kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) kuanzia msimu ujao wa kiangazi.
Amesema mpango huo utatekelezwa mapema iwezekanavyo, ili kutoa fursa kwa Zanzibar kupata wataalamu watakaosaidia maendeleo ya nchi yao katika miaka michache ijayo.
Dr. Rawya pia ameelezea haja kwa Zanzibar kujipanga katika utoaji wa elimu, ili kuwapa wanafunzi elimu iliyo bora na itakayowasaidia kupata ajira baada ya kuhitimu masomo yao.
Hassan Hamad, OMKR.

No comments:
Post a Comment