Msimamo wa Ligi Kuu ya Zanzibar kama inavyosomeka katika ubao uliowekwa katika uwanja wa Mao kuonesha hali halisi ya matokeo na nafasi kila timu.na Picha ya chini wadau wa mchezo huo wakiangalia msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar baada ya mchezo wa Malindi na Mundu.
Kiongozi wa timu ya Malindi Kau akiwa haamini kama timu yake itaibuka na ushindi na kujinasuwa kushuka daraja akifuatilia mchezo huo.
Wapenzi wa mchezo Zanzibar wakiwa wachache wakifuatilia mpira wa ligi kuu ya Zanzibar kati ya Mundu na Malindi.
Mpenzi wa mchezo wa mpira wa miguu Zanzibar Azan Kesi akiwa katika uwanja wa mao akifuatilia mchezo wa ttimu yake ya malindi ikicheza na timu ya Mundu, Azan Kesi alikuwa mshabiki mkubwa wa timu ya Shangani na mpezi wa timu ya Malindi.
Viongozi na wachezaji wa timu ya Mundu wakifuatilia mchezo wao na timu ya Malindi uliofanyika katika uwanja wa Mao timu hizo zinapigania kutoshuka daraja kutokana na kuwa katika nafasi za chini katika ligi hiyo.
Waamuzi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar wakichezesha mchezo kati ya timu ya Mundu na Malindi,kutoka kushoto Ramadhani Kibo amefunguliwa hivi karibuni Mpoma na Mgaza wakitoka uwanjani kwa ajili ya mapumziko.
Kocha wa timu ya Malindi akiwa mkali kutowa maelekezo kwa wachezaji wake kushinda mchezo huo wakati wa mapumziki timu hiyo ilikuwa inaongoza bao 1-0.
Kocha wa timu ya Mundu Juma Mnungwi akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko.
Mchezaji wa timu ya Mundu akiwapita mabeki wa timu ya Malindi katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Mao, timu hizo zikigombea kutoshuka daraja kutokana na kuwa katika nafasi za mkiani.
Mchezaji wa Zamani wa timu ya Malindi Seif , akimuomba samahani Refalii wa mchezo huo Ramadhani Kibo baada ya mchezo kumalizika baada ya kumshambulia kwa maneno wakati wa mchezo huo akidai kuipendelea timu ya Mundu, timu ya Malindi imeshinda kwa 2-1.
0 Comments