Na Mwandishi wetu, Arusha
MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo baada ya jeshi la polisi kutangaza rasmi kwamba mashtaka dhidi yake yamekamilika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu mashtaka dhidi yake yameshakamilika.
"Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili,"alisema Sabas.
Alikamatwa usiku wa kuamkia juzi baada ya polisi kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchomoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika majira ya saa 9:00 alfajiri.
Mbune huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu katika chuo cha uhasubu baada ya kutokea mauaji ya mwanafunzi Henry Koga aliyeuawa kwa kuchomwa kisu wakati akirejea chuoni hapo kutoka kwenye matembezi yake.
Hata hivyo,haijajulikana mara moja sababu za kuawa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.
No comments:
Post a Comment