Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika Mkutano wa Majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Amani Kichama, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa wa Mjini, na kutoa nafasi kwa Wanachama wa CCM kuchangia na kutowa Matatizo yao baada ya ziara yake jana.
Wazee wa CCM Mkoa wa Mjini wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akihutubia katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini Amani.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika mkutano huo wa majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Amani Unguja.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, akisikiliza michango ya Wanachama wa CCM, katika mkutano wake wa Majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Amani Unguja katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa wa Mjini Amani. kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini na kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
Mwanachama wa CCM akitowa mchango wake kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika mkutano wa majumuisho.jumla ya WanaCCM sita wamepata nafasi kutowa michango yao kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
No comments:
Post a Comment