
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akipozi na familia ya Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
PICHA NA IKULU
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS KIKWETE AKUTANA NA NAIBU RAIS WA KENYA WILLIAM RUTO MBUGANI SERENGETI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais
mteule wa Kenya Mhe. William Kipchirchir Samoei arap Ruto ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya
Pasaka.
Akiongea na mgeni huyo katika hoteli
ya Kitalii ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani
Mara, Rais Kikwete amempongeza
Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye
uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Mhe Rais pia alimuelezea Mhe Rutto juu y furaha yake pamoja na kuridhishwa na jinsi
uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.
Alielelezea matumaini yake ya kuwa urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya utadumishwa
pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Mhe Rutto, ambaye aliwasili
mkoani Mara wiki iliyopita akiwa na mke wake na watoto,
ameondoka leo baada ya chakula cha
mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.
Mwisho
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Aprili, 2013
No comments:
Post a Comment