Habari za Punde

Waziri Samia atembelea miradi inayofadhiliwa na SMT

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akifafanua Jambo wakati alipotembelea Mradimpunga wa Umwagiliaji kwenye Bonde la Mpunga la Jendele kulia Mwenyekiti wa Tasaf Jendele Ali Mussa waziri alifanya Ziara ya Wilaya ya Kati Unguja kukutembelea Mradi Uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 Mratibu wa wa Programu ya kuimarisha huduma za kilimo Bw Zaki Khamis Juma akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan kuhusu wakulima wa kuzalisha Mbegu za Mpunga kwenye Bonde la Kinyasini -kisongoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa Ziara ya kutembelea Miradi ya Tasaf na Assp inayofadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akipita kwenye shamba la mpunga la kuzalishia Mbegu la kinyasini-kisongoni Walaya ya Kaskazini A Unguja Waziri akiwa katika Ziara ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na ASSP [Picha na Ali Meja ] 


Na Ali Issa Maelezo Zanzibar 4/4/2013
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu Hassan amesema  kuna umuhimu mkubwa kwa wana nchi kuituza na kuindeleza miradi inayofadhiliwa na Serikali zote mbili  na washirika wa maendeleo ili miradi hiyo indelee kuwanufaisha wananchi na kutimia lengo lililo kusudiwa.
Hayo ameyasema leo huko Jendele wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja wakati alipofanya ziara  kutembelea miradi mbali mbali ya kilimo iliofadhiliwa na TASAF kupitia Serikali ya muungano Tanzania.
Amesema Serikali imekua ikitoa pesa nyingi kufadhili wananchi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa lengo kwamba wananchi hao waweze kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato jambo ambalo baada ya mradi huo kukabidhiwa wananchi husuasua na hatimae kufa kitu ambacho hakifurahishi.
Amesema wana nchi wajifunze kuitunza na kuendeleza miradi hiyo kwani ina umuhimu mkubwa na kuwanufahisha wao wenyewe.

 “Kuiacha miradi ife si vizuri ,muichangie iliijiweze kujiendesha na huko ndio faida ya miradi hiyo”.alisema Samia.
 Aidha Waziri aliwambia wakulima wa bonde la jendele Kinyasini Kisongoni wajitume kwa kuzalisha kwa wingi chakula kwani sasa hakuna sababu kwa  vile maji yapo ya kutosha katika bonde hilo hivyo  uzalishaji uongezeke.
 Waziri hoyo alisema dhamira ya ziara yake kuja Zanzibar ni kuona vipi matumizi ya pesa za TASAF zinavyotumika katika miradi iliyoombewa na utekelezaji wake umefikiaje kwa wananchi.
 Waziri alifurahishwa na juhudi zinazochukuliwa kwani kumefikiwa hatua kubwa za kumaendeleo na zinatia moyo kwa matumaini .
 Waziri alitembelea mradi wa  mpunga wa umwagiliaji maji jendele na mradi wa uzalishaji mbegu za mpunga kinyasini kisongoni na badae kupata maelezo juu ya miradi ASSP na SPDL inayo endeshwa na wizara yakilimo na maliasili na ushirika Zanzibar .
 Miradi hiyo kwa TASAF ya awamu ya kwaza Zanzibar   ilipatiwa dola za kimarekani milioni tatu ambapo ziligawiwa sawa sawa kwa unguja na pemba.
 Awamu ya pili TASAF Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani 2,500.000.00  ambapo zilitumika kumalizia mradi wa kwaza unguja na pemba kupitia mifuko mitatu nayo ni mfuko wa Taifa wa kijiji (NVF) wenye thamani ya fedha TShs 2,500,000,000.00,mfuko wa mradi wa ukanda wa Bahari (MACEMP) wenye thamani ya fedha TShs 1,800,000.000.00
 Ziara hiyo itaendelea kesho kutembelea idara ya uhamiaji Zanzibar na mamlaka ya kitambulisho cha Taifa Zanzibar.  
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.