Habari za Punde

Dk Shein azungumza na wanafunzi mjini Nanjing, China

 Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Elimu za Juu katika Vyuo Vikuu katika Mji wa Nanjing Jimbo la Jiangsu nchini China,wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Sofitel Luxury Hotel,katika mazungumzo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Elimu za Juu katika Vyuo Vikuu katika Mji wa Nanjing Jimbo la Jiangsu nchini China,wakisikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) wakati alipozungumza nao leo katika ukumbi wa mikutano wa Sofitel Luxury Hotel, Mjini Nanjing katika jimbo la Jiangsu akiwa katika ziara ya Kiserikali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akiwa na Mama Mwanamwema Shein,kushoto pamoja na Mawaziri na Maofisa aliofuatana nao katika ziatra ya Kiserikali nchini China,Rais alipata muda wa kuzungumza na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma katika Vyuo Vikuu mbali mbali, na aliwaelezea hali halisi ya Utulivu na Amani Iliyopo nchini Tanzania ambapo aliwataka kuondokana na wasiwasi
Mwanafunzi Sauli Elingarama ,Dkt wa Bianadamu aliokuwa akiuliza suali mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa mazungumzo na Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Vyuo Vikuu vya Mji wa Nanjing Nchini China katika jimbo la Jiangsu,Rais yupo China kwa ziara ya kiserikali.[Picha na Ramadhan Othman China.]

2 comments:

  1. Loooo.. Kweli Dhulma ya Elimu ya Juu na Scholarship za nje iko wazi wazi kabisa..

    Wanafunzi hao wote ni kutoka Bara -Tanganyika na inaonekana hamuna Muislamu hata mmoja ..Isipokua yule msichana aklievaa hijabu ... Pengine atakua ni mtoto wa Mkubwa fulani anaetumikia Mfumo Kristo wa Muungano...

    Kama kuna mtu atanisuta naomba aniwekee majina ya Wanafunzi hao.

    Tutapata wapi nafasi za masomo ya juu ikiwa Watoto wetu na Nduguzetu Waislamu wa Tanganyika wanapewa Divission 4 au Wanafutiwa matokeo?..

    Tumeona matokeo ya kidato cha 4 jinsi yalivyochakachuliwa.. Watoto wenye Akili ni Wabara tena ni Wakristo tu.. Waislamu wanaonekana hawana akili.

    ReplyDelete
  2. Angalia vizuri waliovaa hijabu hapo ni mke wa Dr. shein na msaidizi wake.

    Wewe unashangaa matokeo ya Form 4, hebu angalia na ya Form 6 ndio utachoka!

    Mambo haya ukianza kuyajadili usipokua makini unaweza ukafa, kwasababu yana sababu nyingi ukiwemo uzembe wetu wenyewe wa kusimamaia elimu visiwani.

    Tulitakiwa sisi tuweze kusimama kwa miguu yetu kwanza ndio baadae tuwasaidie ndugu zetu wa Tanganyika.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.