Habari za Punde

Jumuiya za CCM kuwajengea uwezo vijana kujinasua na hali ngumu ya kimaisha

 Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walioshiriki katika Mkutano wa Jumuiya za UVCCM, UWT na Wazee. Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui.
 Mwandishi wa Gazeti la Habari Leo Khatib Burecha akiuliza swali katika Mkutano wa Waandishi wa habari na Jumuiya za UVCCM, UWT na Wazee. Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui
Naibu Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania UWT Salama Aboud Talib akifafanua jambo katika Mkutano wa Jumuiya za UVCCM, UWT na Wazee na Waandishi wa habari. Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya CCM Zanziba Kisiwandui
 
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 15/5/2013
Jumuiya za Chama cha Mapinduzi UVCCM, UWT na Wazazi zinakusudia kuwajengea uwezo Vijana ili kujinasua na hali ngumu ya kimaisha kwa kuwasomesha kupitia Skuli za Wazazi na Elimu ya Amali ili waweze kujiajiri wenyewe.
Zimesema Vijana watakapopata Elimu hiyo itawasaidia kuweza kujiajiri na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira linaloendelea hapa Nchini.
Naibu Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania UWT Salma Abuod Talib ameyamesa hayo huko Makao makuu ya CCM Zanzibar Kisiwa nduwi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kwa lengo la kupongeza mafanikio ya ziara ya kichama iliyofanywa na Dkt. Shein.
Amesema Mafunzo ya Amali yatawasaidia Vijana kuondokana na fikra za kutegemea Ajira kwa Serikali na kuwawezesha kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea Serikali.


Akizungumzia ziara hiyo Bi Salma amesema ziara ya DKT Shein imekuwa na mafanikio makubwa kwani imeweza kuongeza Wanachama wapya jambo ambalo ni ishara ya wazi ya uhai na matumaini ya ushindi wa Chama hicho katika Chaguzi za badae .
Amesema katika hali hiyo kuna haja kubwa kumpongeza kiongozi hiyo kwani imetoa picha ya kufanikiwa kukiimarisha chama na kukiletea maendeleo hapa visiwani na Tanzania kwa ujumla.
“Jumuiya za chama cha mapinuzi (UVCCM , UWT na Wazazi) Tuna mpongeza kwa dhati kabisa kuwa Mjasiri wa kutembea bila kuchoka na kuwa tayari kutumika kila ambapo alitakiwa ushiriki wake, inaonesha wazi kuwa Makamu Mweneyekiti wetu ni mtu wa watu na anapenda watu pamoja na maendeleo yao”amesema Bi Salma.
Aidha alisema katika ziara hiyo DKT Shein alikagua na kutembelea miradi ya CCM ambapo miradi 35 iliwekewa jiwe la msingi na kuziduliwa ikiwemo SACCOS mbali mbali na Vikundi vya Ushirika .
Akizungumzia sintofahamu iliyopo katika baadhi ya Majimbo Bi Salma alisema CCM imepanga kufanya vikao vitakavyojumuisha Viongozi wa Majimbo wakiwemo Wabunge na Wawakilishi pamoja na Wananchi wao ili kuimarisha uttendaji wao
Amesema Vikao hivyo vitatoa mustakabali nzuri kwa Viongozi hao na kuweza kuwatumikia Wananchi waliowachagua katika hali inayofaa.
Jumla ya Wanachama wapya 5,448 kutoka Vyama mbali mbali vya Siasa wamejiunga na Chama cha Mapinduzi kufuatilia Ziara ya Makamo Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Ali Mohammed Shein aliyoifanya karibuni kutembelea Mikoa mitano ya Unguja na Pemba kwa lengo la kuangalia na kukipa uhai chama cha Mapinduzi na jumuiya zake.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 15/5/2013

1 comment:

  1. Wambieni ukweli vijana msiwatafunie maneno, hakuna ajira ya upendeleo kwa kuwa tu, kijana ni mwanachama wa CCM. wajithidi kusoma kufa na kupona elimu sasa ni jihadi!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.