WATOTO WA KUNDEMBA BAADA YA KURUDI KUSAKATA KABUMBU UWANJA WA RIO DE JANAIRO.
Hawa ni baadhi ya wachezaji niliokutana nao wa mbele ni Abuu Sinyo kitoto machachari cha Kundemba.
Hiki ndicho kizazi kipya kilichozaliwa mtaa wa Kundemba na kujikuta kimezaliwa katika wimbi la madawa ya kulevya yaliobobeya ndani ya mtaa huu ambao ulikuwa na sifa nyingi za kupendeza miaka ya nyumba kabla ya kuathirika na madawa.
Harakati za maisha katika kukinusuru kizazi hiki kuingia katika dimbwi hilo ni kuwapa sapoti vijana hawa kwa kuwachangia vifaa katika timu yao na kuwa na kauli mbiu kwamba 'Kundemba bila ya madawa ya kulevya inawezekana'
Madawa ya kulevya imekuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi wa hali duni hasa kutokana na kuangamizwa vijana wao na familia zao kwa utumiaji wa madawa haya.
Kibaya zaidi ni kwamba biashara hii imeshaota mizizi ya ukubwa wa mbuyu hivyo kutaka kui'ngoa kunahitajia mtu kuwa jasiri, shupavu na aliyekabidhiwa zana zote za kuhakikisha mbuyu una'ngoka, shughuli ambayo ni pevu lakini inawezekana kama kutakuwa na dhamira ya kweli.
Mtaa wa Kundemba, kwa wasioujua upo katika Wilaya ya Mjini shehia ya Mwembeladu na umepakana na mitaa ya Baraste kipande, Mbuyu pacha, Rahaleo na Kwa haji tumbo. Ulikuwa na timu ya mpira maarufu kama Kundemba Shooting Stars na pia miaka ya sabini ilisifika kwa kuwepo klabu ya beni ya mbwa kachoka, na miaka ya themanini na tisini kwa ngoma ya Chakacha.
Inasikitisha kuona vijana wengi wa mtaa wa Kundemba walioathirika hawana thamani, wala maadili, wamepoteza utu wao, wameitupa haiba yao wamekuwa tegemezi baada ya wao kutegemewa.
kadri tutakavyolizungumzia suala la madawa ya kulevya hatuwezi kulimaliza wala kulipatia ufumbuzi wa haraka kwani hatuna uwezo huo kwani shina tayari limeshakuwa na matawi mengi kwenda juu na mizizi imeshakuwa mikubwa sana kwenda chini.
Lakini tukianza kuhamasisha kizazi kinachokuja mapema sana kwa kukipa uwezo wa kubaini madhara ya madawa ambayo wakizaliwa tu tayari hukabiliana nayo mitaani na kuwapa uwezo wa kutafuta njia za kujiepusha wao wenyewe pamoja na kujenga mustakabali wao wakiandaliwa na kuwezeshwa kwa kupewa mbinu za kutokomeza madawa haya , niaamini tunaweza kuwa ni mwanzo mzuri kuelekea kutokomeza janga hili mtaani Kundemba.
Tuwape sapoti vijana hawa na kuwapa matumaini.
Ewe Mola kinusuru kizazi hichi na madhara ya madawa hayo na mengineyo. Amin.
ReplyDeletePia wadhalilishe wote wanaoingiza madawa hayo katika visiwa vyetu, na wenye mamlaka ya kuzuia ambao wanajishughulisha na kuwachia kwa makusudi uingiaji wa madawa hayo.
Kinga ni bora kuliko tiba.
Kule Nchi za Wenzetu Zilizokua Hazitawaliwi na Wafalme Weusi (Mabepari Mambo Leo) Watoto kama hawa hua wako katika timu za Joniur na Wanakua wanatayarishwa kuchukua nafasi za National Timu wanapotimia miaka 18-19.
ReplyDeleteLakjini kwetu hakuna National timu wala mavi gani.. Utakuta Vibunju vya KMKM, au Baraza la Uwakilishi wanaburuza Matumbo yao Uwanjani ati ndio Timu za Mpira wa Miguu huo. Huku Wakiwaacha watoto wetu wanagaragara mitaani bila yakwenda shule au kua na Msingi wa Maisha.
Ndio hivyo tena hutumwa na dawa za kulevya na baadae wakawa Wateja na Wananunuzi. Who care as long As Italian bought a beutifull beach in Zanzibar for the next 100 years.. Who really borther about the children of Slave....
Tutabakia hivi hivi kwa unafiki wetu na kubaguana wenyewe kwa wenyewe.. Sijui weye CUF ..sijui weye Mpemba.. Sijui weye Muislamu.. n.k