Na Waandishi wetu
HATIMAYE bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, imepita baada ya kufanyiwa marekebisho.
Bajeti hiyo ilirejeshwa juzi ili kutoa nafasi kwa wizara na kamati ya viongozi wa kitaifa ya Baraza la Wawakilishi, kuipitia upya.
Wawakilishi walikubali kuipitisha bajeti hiyo baada ya Waziri, Fatma Abdulhabib Fereji kufafanua jinsi fungu la Tume ya Ukimwi ambalo ndio lililozua mjadala, lilivyofanyiwa masahihisho.
Mapema Mwenyekiti wa Kamati , Hamza Hassan Juma, alisema kamati yao kwa kiasi kikubwa imeridhika na masahihisho yaliofanywa.
Akitoa maelezo yake baada ya ufafanuzi huo Mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu alisema ,ingawa kumefanyika masahihisho katika fungu hilo, lakini kutahitajika uwepo umakini kwa kamati za baraza pale watapokuwa wanapitia matumizi ya wizara.
Alisema kinachoonekana katika matumizi ya serikali baadhi ya watendaji hupanga matumizi yenye utata, kwani hata baadhi ya hoja wakati walipokaa katika kamati hiyo kuna mambo yalionekana kutokuwa na majibu.
Mwakilishi huyo, alimpongeza waziri wa wizara hiyo kwa kukubali kufanya ufafanuzi juu ya hoja ambazo zilionekana kuwa na utata.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alisema serikali inakubaliana na jitihada zilizochukuliwa na viongozi wa Baraza la Wawakilishi kwa dhamira ya kuimarisha utawala bora.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, aliipongeza hatua ya Mwakilishi huyo kutambua baadhi ya maeneo yenye utata.
Kuhusu fedha za vifaa zilizotengwa kwa ajili ya Pemba, alisema ni kweli fedha hizo ni nyingi kutokana na fisi zimechoka na hazina vifaa na kama kuna wasi wasi utaweza kuondolewa kwani.
Hata hivyo, Waziri huyo alimtaka Mwakilishi huyo kukubaliana na baadhi ya hoja kwa vile nia ya serikali ni kuhakikisha kuwanakuwa na matumizi bora ya serikali.
Aidha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, aliipongeza hatua ya Mwakilishi huyo kuweza kutambua baadhi ya maeneo ambayo yalionesha kuwa na wasi wasi nayo.
Mapema Spika, Pandu Ameir Kificho amezitaka Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi kufanya kazi kwa makini zinapopitia bajeti za wizara ili kuondoa kasoro zinazojitokeza.
Akizungumza wakati akiahirisha kikao cha baraza jana asubuhi, kufuatia juzi wawakilishi kukataa baadhi ya vifungu katika bajeti ya ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Spika Kificho alizitaka kamati hizo ziwe makini.
Alisema kutofanya kazi ipasavyo kwa kamati hizo ndiko kunakosababisha kukwamisha baadhi ya vifungu vya matumizi ya fedha wakati wa kujadiliwa.
Spika alisema kamati zina jukumu kubwa la kuhakikisha wanaichunguza bajeti pamoja na kuitoa kasoro zote ambazo zitajitokeza kabla ya kuwasilishwa barazani kujadiliwa.
“Kamati mnapoletewa hotuba ya bajeti mhakikishe kwamba mnaipitia kwa makini ili wajumbe wanapokuja kuipitisha kusiwe na kasoro,” alisema.
Aidha alisema waziri anaehusika lazima ahakikishe anatoa vizuri majibu ya masuala yote yanayoulizwa na wawakilishi.
“Mawaziri mnapokuja kuwasilisha hotuba za bajeti zenu mhakikishe mnajua kila kitu kilichomo ndani yake kwa kuwauliza wasaidizi wenu kama Makatibu na wengineo ili mnapoulizwa mtoe ufafanuzi sahihi,”alisema.
Alisema kuchelewa kupitishwa bajeti ya ofisi ya Makamu wa Kwanza kumeanza kuathiri muda wa kikao hicho na si busara kwa baraza la wawakilishi kutumia fedha zilizo nje ya matumizi. (habari hii imeandikwa na Mwantanga Ame, Kauthar Abdalla na Asya Hassan).
Rais Samia Aelekeza Ushirikiano kati ya Makampuni ya Madini na Chuo cha VETA
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
ameyaelekeza makampuni ya madini kuchangia na kushirikiana na chuo cha VETA
Geita katika ...
1 hour ago
Samahani sana Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Ili iris wa bila ya kufanyiwa
ReplyDeletecoyote . Ni muhimu kuweka taarifa kwa usahihi tujitahidi kupata taarifa kwa usahihi wake