Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi khamis, alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akitokea ziarani Nchini China alipokuwa na ziara ya Kiserekali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee waliofika kumpokea uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiwa na Kiongozi wa Brass Bendi ya Chipukizi, wakati wa mapokezi yaliofanyika katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiangalia ngoma ya Kikundi cha Vijana kutoka amani wakicheza burudani kwa Rais wa Zanzibar Dk. Shein alipowasili Zanzibar akitokea ziarani China .
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na ziara yake Nchini China, akiwa katika ukumbi wa VIP uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akizungumza na waandishi mafanikio ya ziara yake Nchini China.
Viongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar waliokuwa katika msafara wa Rais wa Zanzibar Nchini China wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk. Shein, akizungumza na waandishi wa habari alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Wasanii wa Kikundi cha Vijana wa Amani wakitowa burudani ya ngoma ya Kibati wakati wa mapokezi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akitokea ziarani nchini China.
Haya, wahadimu wamesharudi China, sasa watuoneshe hicho walichojifunza tena kwa vitendo.
ReplyDeleteManake walikwenda 'kijiji kizima' huku akina Mh. Ramadhan Abdalla Shaaban wakicha mafaili mengi ya uhaulishaji mezani kwao.
Mchekeshaji mkuu wa Rais Mh Abdalla Mwinyi. naona nae yupo kazini
ReplyDelete